Mtanzania Mbelwa alipocheza ngumi Afghanistan
*Pambano lawa gumzo katika nchi
KABUL
MTANZANIA Said Mbelwa, alipoteza pambano dhidi ya bingwa wa ngumi wa Afghanistan Hamid Rahimi, ambalo lilitazamwa na mashabiki wengi kwenye kwenye televisheni.
Pambano hilo la ngumi za kulipwa lilifanyika kwa lengo la kuhamasisha amani katika nchi hiyo ambayo imekuwa ikikabiliwa na vita, liliisha katika raundi ya saba baada ya Mbelwa kuacha kupigana kwa kudai ameumia bega.
Rahimi ambaye alizaliwa Afghanistan na kukulia Ujerumani na Mbelwa walitwangana kuwania ubingwa wa Mabara wa WBO uzani wa Middle.
HIlo ni pambano la kwanza la ngumu za kulipwa kwa Rahimi kulicheza katika nchi yake aliyozaliwa
Wakati mamilioni ya mashabiki waliangalia pambano hilo kupitia chaneli mbili za televisheni ikiwemo inamilikiwa na serikali ya Afghanistan yaRTA, mamia ya watu wakiwemo maafisa wa juu, wanasheria na mabalozi walijumuika katika ukumbi wa Loya Jirga mjini Kabul uliokuwa na ulinzi mkali kushuhudia pambano hilo.
Kiingilio cha pambano hilo kilikuwa dola 50 (zaidi ya sh. 75,000) na dola 100 (zaidi ya sh. 150,000).
Rahimi alipata ushindi raundi ya saba baada ya Mbelwa kudai ameumia shingo.
Akizungumza baada ya mechi, Rahimi alisema, " Mkanda huu si wangu, huu mkanda ni wa Afghanistan. Ni wenu. Ninawapenda," Rahimi alikuwa na furaha jukwaani aliwaambia mashabiki.
Pambano hilo lililopewa jina "Fight 4 Peace," (Pambano kwa Amani) lilikuwa tukio kubwa katika nchi hiyo ambayo imekuwa ikipata maisha mapya niaa ya awali kuwa chini ya Taliban, awali ilionekana kama pambano hilo lingezuiwa.
Wataliban waliongoza nchi hiyo kati ya mwaka 1996 na 2001, na kuzuia raia wengi kushiriki katika shughuli nyingi za kijamii ambazo zinaonekana ni kinyume na Uislamu.
Uwanja mkubwa wa michezo uliopo Kabul, Ghazi ulikuwa ukitumika kwa kama uwanja wa kuwanyonga watu hadharani na kuwapiga watu waliotiwa hatiani kwa uhalifu katika miaka ya 1990.
"Nina uhakika hakuna mmoja kati ya (wapiganaji) wawili angethubutu kuingia nchini, kama Taliban wangekuwa bado wanaendelea. Nimesurahi sana kwamba sasa tunasonga mbele katika sehemu ambayo dunia inatutambua," Sayed Ahmad Peerzada, ambaye ni muuza duka ali.iambia Shirika la habari la Marekani, CNN.
Tukio hilo lilitawala katika vyombo vya habari vya kijamii ambapo watu wengi walikuwa wakiandika katika mitandao ya Twitter na Facebook kuonesha wanafuarahia kuwepo kwa mechi hiyo.
Tukio hilo lilimgusa hata Rais wa nchi hiyo, Hamid Karzai ambaye alitoa salamu kutoka Ikulu yake mjini Kabul kuwapongeza mabondia wote wawili.
"Rais, Mbalia ya kumpongeza Rahimi, anamshukuru mpinzani wake kutoka Tanzania ambaye alikuja Afghanistan kushiriki pambano hili," Taarifa kutoka ofizi ya Karzai ilisema.
Rahimi Alizaliwa Afghanistan mwaka1983 alitoroka kwenda Ujerumani akiwa na famiulia yake mwaka 1992 baada ya nchi yake kutawaliwa na vita ya wenywe kwa yenyewe.
Ana rekodi ya kushinda mapambano 20 kati ya 21.
No comments :
Post a Comment