Jeshi
la polisi wilayani Makete mkoa wa Njombe linamshikilia Bi Rose Skwea
Tweve mkazi wa kijiji cha Isapulano kwa tuhuma za kummwagia maji ya moto
mke mwenzake Estina Kristian Sanga [23] pamoja na mtoto wake mdogo
ambao wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Makete kwa matibabu zaidi.
akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo mrakibu wa polisi ambaye pia ni afisa upelelezi
(OCCID) wilaya ya makete Gosbert Komba amesema matukio ya kujichukulia
sheria mkononi yamekuwa yakijirudia mara kwa mara wilayani hapo huku
akiwataka wananchi kufuata sheria na taratibu za nchi.
kwa
upende wake Bi Estina Sanga Ambaye amejeruhiwa na mke mwezake huyo
amesema kuwa tukio hilo lilimpata majira ya saa mbili usiku alipokuwa
anakwenda kumjulia hali mume ambae ni mgonjwa nyumbani kwa Bi Rose
ambaye ni Bi mkubwa.
Naye
mtuhumiwa wa tukio hilo Bi Rose Tweve amesema alifikia hatua hiyo baada
ya kurushiana maneno na mke mweziye huyo na kuchukizwa kwa kitendo cha
kwenda kumuona mume wao huku akiwa amelewa ndipo akachua sheria mkononi
kwa kumwangia maji ya moto ka njia ya kumuonya.
akizungumzia
tukio hilo Bwana Itiso Chaula (32) ambaye ni mume wa wanawake hao mkazi
wa kijiji cha Isapulano amesema ameshangazwa na tukio ambalo Bi mkubwa
amelifanya kwa Bi mdogo na kulaani kitendo hicho.
Occid Komba amesema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi huku upelelezi ukiendelea, lakini amesema kwa taarifa alizonazo majeruhi anaendelea na matibabu baada ya kujeruhiwa na maji moto usoni na maeneo ya kifuani
NA EDWIN MOSHI, GLOBU YA JAMII MAKETE
No comments :
Post a Comment