Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, October 11, 2013

HABARI ZA MICHEZO, BURUDANI SASA KUPATIKANA KUPITIA SIMU ZA MKONONI


Meneja wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Push Media Mobile, Rugambo Rodney (kulia) akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya kupata taarifa mbalimbali zikiwa pamoja na michezo ijulikanayo kwa jina la SIMU TV wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo jana.Ili kuweza kupata huduma hiyo, unatakiwa kutuma neno SIMUTV kwenda namba 15678 na kufuata maelekezo. Kulia ni meneja mahusiano wa Push Media Mobile, Ezekiel Mukundi.
******************************************************
Na Mwandishi wetu
Watanzania sasa wanaweza kupata taarifa mbali mbali zikiwa pamoja na za michezo, burudani kupitia simu ya mkononi baada ya kampuni ya Push Mobile Media kutambulisha huduma mpya ya simu tv.
Meneja wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Push Media Mobile, Rugambo Rodney alisema kuwa ili kuweza kupata huduma hiyo, unatakiwa kutuma neno SIMUTV kwenda namba 15678 na kufuata maelekezo ili kupata huduma hizo ambayo pia inapatikana kwa kupitia njia ya mtandao www.simu.tv.
“Tumeamua kuanzisha huduma hii ili kuwawezesha watanzania kupata taarifa mbali mbali mbali moto moto kwa njia ya urahisi zaidi kupitia simu zao za kiganjani,” alisema Rugambo.
Rugambo alifafanua kuwa mbali ya huduma za michezo na burudani, pia watanzania wanaweza kupata taarifa nyingine kama nyimbo za Qaswida, nyimbo za injili, filamu, siasa, uchumi, Taarifa za habari, nyimbo mbali mbali kwa njia ya video na biashara kwa kupitia simu zao za mikononi.
Alisema kuwa huduma hiyo ni ya kwanza hapa nchini na pia inawawezesha watumiaji kuona vipindi mbali mbali vinavyorushwa na vituo vyote vya televisheni zote hapa nchini na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa huduma imetengenezwa kuwapa watumiaji picha nzuri na zenye ubora wa hali ya juu, ambazo zimetengenezwa maalumu kwa ajili ya simu za mkononi.

No comments :

Post a Comment