Na Mwandishi Wetu
Bendi
ya taarabu ya Mashauzi Classic kesho (Jumatano) itatambulisha nyimbo
zao mpya kwenye onyesho maalum ya kusherehekea sikukuu ya Idd el Hajj
katika ukumbi wa Dar West Park, Tabata.
Onyesho
hilo ambalo linajulikana kama ‘Usiku wa Isha Mashauzi’, imeandaliwa na
Keen Arts na Bob Entertainment chini ya udhamini wa kinywaji cha
Konyagi, Straika, Kwetu Mbambabay na Saluti5.
Mratibu
wa onyesho hilo, Joseph Kapinga amesema kuwa onyesho litakuwa la
kipekee na maalum kwa kusherehekea sikukuu ya Idd El Hajj.
Amesema
katika onyesho hilo, Mashauzi atatambulisha albamu yake mpya
ijulikanayo kama “Asiyekujua Hakuthamini” ambayo ina nyimbo kama “Mimi
Bonge la Bwana,” utunzi wake Hashim Said, “Ropokeni Yanayoyahusu” (
Saida Ramadhani) na “Haya ni Mapenzi Tu” (Zubeda Malik).
Zawadi mbalimabli zitatolewa kwa mashabiki wa bendi hiyo inayojulikana kama Wakali wa Kujiachia.
“Tumeandaa
zawadi mbalimbali kwa mashabiki wetu. Pia bendi ya Mashauzi Classic
watatumia onyesho hilo kutambulisha nyimbo zao mpya,” Kapinga alisema.
“Mashauzi
Classic watapiga albamu zao zote. Matumaini yetu ni kuwa watu watapata
burudani ya kutosha kuliko siku zingine zote,” alisema Kapinga.
Nyimbo
zingine zitakazopigwa ni “Viwavijeshi” (Issa Ramadhani), “Sitasahau
Yaliyonikuta” (Abdul Malik), “La Mungu Halima Mwamuzi” (Zubeda Malik) na
“Sijamuona Kati Yenu” (Rukia Juma).
Naye
mkurugenzi wa bendi hiyo, Isha Mashauzi, alisema kuwa onyesho la Da
West litakuwa la kihistoria na kutaka watu wajitokeze kwa wingi ili
historia isiwapite.
“Kwa kweli bendi iko fiti,” alisema Mashauzi.
No comments :
Post a Comment