Rais Kikwete akikaribishwa kutembelea Jengo la Bunge mjini Dodoma na Naibu Spika Mhe. Job Ndugai leo Oktoba 24, 2013.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Alhamisi, Oktoba 24, 2013 ametembelea na kukagua Jengo la Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma kujionea maandalizi ya
jinsi Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba watakavyokaa katika Ukumbi wa
Bunge hilo.
Bunge
hilo Maalum la Katiba litakuwa na Wabunge 600 tofauti ya Bunge la sasa
lenye Wabunge 354 ambao ni pamoja na Wabunge 239 wa kuchaguliwa kutoka
majimboni, Wabunge Wanawake Viti Maalumu 102, Wabunge wa kuteuliwa toka
Baraza la Wawakilishi Zanzibar 5, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na
Wabunge 7 (kati ya 10) wa kuteuliwa na Rais.
Rais Kikwete akiangalia sehemu ya viti ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo Oktoba 24, 2013.
Rais Kikwete akitembelea Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo Oktoba 24, 2013.
Rais
Kikwete akisindikizwa na Naibu Spika Mhe Job Ndugai na Katibu wa Bunge
Dkt Thomas Kashilila baada ya kutembelea Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma
leo Oktoba 24, 2013.
Rais
Kikwete akizungumza na Naibu Spika Mhe Job Ndugai na Katibu wa Bunge
Dkt Thomas Kashilila baada ya kutembeleaUkumbi wa Bunge mjini Dodoma leo
Oktoba 24, 2013. PICHA NA IKULU
No comments :
Post a Comment