Washindi
wa shindano la Biggest Baddiest Bascket, Allex Ayling (kushoto) na
Mwenzake Mark wakitembezwa na kuangalia namna walemavu wa kituo cha
Shanga River House cha jijini Arusha, washindi hao waliopatikana kupitia
kampuni ya My Destination walikuwa nchini na kutembelea vivituo
mbalimbali vya utalii na kukagua miradi mbalimbali kama hiyo.
Mshindi
wa shindano la Biggest Baddiest Bascket, Allex Ayling akipuliza kioo
kilicho yeyushwa tayari kwa kutengenezwa chombo chochote ambavyo
hutokana na taka ngumu zinazozalishwa na binadamu ikiwa ni moja ya
shughuli zinazo fanywa na walemavu katika kituo cha shanga river house
cha jijini Arusha.
Allex na Mark wakipewa maelezo ya shughuli za kituo.
WADAU mbalimbali wa utalii wa ndani na nje ya nchi wametakiwa kuutangaza utalii wa Tanzania katika maeneo yao ili kuwavutia watalii wengine kuzidi kufika kwa wingi hapa nchini kujionea maliasili zilizopo na kuchangia pato la taifa kwa ujumla.
walipewa zawadi na marafiki mbalimbali.
Hayo
yalielezwa jana na Afisa Mtendaji wa TATO ,Sirili Akko wakati
akizungumza na wadau wa maswala ya utalii waliohudhuria katika hafla ya
kuwapongeza vijana wawili walioshinda shindano lililoandaliwa na
kampuni ya My Destination lililoshirikisha washiriki 122 ulimwenguni.
Aidha alisema kuwa ,Tanzania ni nchi ambayo imebahatika kupata vivutio mbalimbali vya utalii hivyo kuwavutia watalii kufika na kujionea maliasili zetu, hivyo hawana budi kuutangaza utalii wetu katika nchi zao ili kuendelea kukuza utalii zaidi kwa nchi za Afrika.
Alisema
kuwa, shindano hilo lilihusu mshiriki kuchagua vitu ambavyo wangependa
kufanya maishani kabla hawajafa ndipo vijana hao wawili waliposhiriki
katika shindano hilo na kuoanisha kuwa wao wangependa kutembea dunia
nzima na kujionea maajabu yaliyopo katika vituo mbalimbali.
‘baada
ya vijana hao kushiriki shindano hilo walishinda na kupewa nafasi ya
kuchagua kutembelea nchi 25 kati ya 80 ambazo katika hizo nchi 25
walichagua nchi tatu za Afrika ikiwemo kutembelea Tanzania,Zimbabwe,na
Afrika ya kusini na ndo maana wapo hapa leo tayari kwa kuanza zoezi
hilo’alisema Akko.
Aliongeza
kuwa, kitendo cha wao kuchagua Tanzania kati ya nchi 25 kimewafariji
sana wao kama wadau wa utalii kwani imeonyesha jinsi ambavyo utalii wa
nchi yetu unaweza kutangazwa na watalii mbalimbali na hatimaye kuweza
kupata wageni wengi zaidi kwa kujionea maliasili zilizopo katika maeneo
yetu.
Nao
vijana hao walioshinda shindano hilo kutoka Calfonia Alex Ayling na
Mark Ayling walisema kuwa, shindano hilo waliweza kushinda baada ya
kukithi viwangovya shindano hilo na hatimaye wamefurahia sana kushinda
kwani mchuano uliwashirikisha watu mbalimbali ulimwenguni.
Alex
alisema kuwa, lengo la kuchagua Tanzania miongoni mwa nchi tatu za
Afrika ambazo wangependa kutembelea ni kutokana na uoto wa asili uliopo
katika maeneo mbalimbali ikiwemo hifadhi ya Serengeti kwa ajili ya
kujionea wanyama mbalimbali kama sehemu ya uchaguzi wao
Alisema kuwa,katika maeneo hayo yote watakayotembelea watakuwa wakichukua mikanda mbalimbali kwa ajili ya kuirusha kwenye mtandao na hatimaye watu mbalimbali kuweza kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo katika vituo watakavyotembelea.
Mark
alisema kuwa, wamekuwa wakifuatilia vitu mbalimbali vinavyoendelea
Tanzania ikiwemo wanyama mbalimbali wa kuvutia , pamoja na kufuatilia
makabila ya wamasai ambayo watakuwa na nafasi ya kuwatembelea na kuweza
kujifunza maswala mbalimbali kutoka kwao.
No comments :
Post a Comment