Redds Miss Tanzania 2012 ambaye pia ni Miss Sinza 2012, Brigitte Alfred (wa kwanza kushoto) akiwa katika pica ya pamoja na Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga (wa pili kulia), Miss Tanzania wa sasa Happiness Watimanywa na Mama wa Brigitte Veridiana Mashingia wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa sherehe ya kupongeza (Brigitte) kwa kushinda nafasi ya tatu ya taji la dunia la kipingele cha urembo wenye malengo maalum. Mrembo huyo aliwashinda warembo 127.Sherehe hiyo ilifanyika kwenye hotel ya Giraffe Ocean mwishoni mwa wiki.
Mwandishi wetu
Redds
Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred Lyimo amesema kuwa ushindi wake wa
nafasi ya tatu katika kipengele cha urembo wenye malengo maalum katika
mashindano ya Miss World mwaka huu ni wa Watanzania wote.
Brigitte
alisema hayo katika hafla ya kuagwa iliyoandaliwa na waandaaji wa
mashindano ya urembo nchini, kampuni ya Lino International Agency
iliyofanyika kwenye hotel ya Giraffe.
Alisema
kuwa amefarijika sana kushinda nafasi hiyo kwani ilishirikisha warembo
wote walioshindana mwaka huu katika mashindano hayo. Alisema kuwa hakuwa
kazi rahis kushika nafasi hiyo kwani kipengele hicho ushirikisha
warembo wote.
“Namshukuru
mama yangu, Verdiana Mashingia ambaye alikuwa bega kwa began a mimi
katika kuhakikisha mradi wangu wa ujenzi wa bweni la albino wa shule ya
smingi Buhangija shinyanga unafanikiwa, pongezi pia kwa kamati ya Miss
Tanzania na wadhamini, Redds,” alisema Brigitte.
"Ndoto
zangu za kuitumikia jamii hazitaishia hapa, nitaitumikia na nitaendelea
kuwasaidia Albino ambao wamenichagua kuwa barozi wao," alisema mrembo
huyo.
Aidha
Brigitte alimpongeza Hapiness na kumtaka atumie kipaji alichonacho na
urembo wake wa asili kuitoa kimasomaso Tanzania kwenye mashindano ya
mwakani.
Mkurugenzi
wa Lino International Agency, Hashim “Uncle” Lundenga alisema kuwa
Brigitte amefanya kitu cha kihistoria Tanzania na kuzishinda nchi kubwa
mbali mbali kama Uingereza, Ufaransa na nyingine nyingi.
Lundenga
alisema kuwa wamefarijika kwa mafanikio hayo na ndiyo maana wameamua
kufanya hafla hiyo ambayo ni ya kihistoria huku akiwapongeza wadhamini,
Redds kwa kudhamini hafla hiyo.
Alisema
kuwa ni vigumu kuamini, lakini ukweli unabaki pale pale kuwa fai yao
inazidi kukuwa, tena kwa mafanikio tofauti na watu wanavyodhani.
“Mfano
mzuri ni mama yake Brigitte alivyokuwa bega kwa bega wakati wote
mwanaye alivyokuwa na taji, huu ni mfano wa kuigwa na tunaomba wazazi
wafuate nyayo za mama huyu,” alisema Lundenga.
Lundenga
alisema kuwa Brigitte ameleta changamoto kubwa kwa mrembo wa sasa
Happiness Watimanywa katika mashindano yanayofuata ya urembo ya dunia.
"Brigitte
amefanya vizuri japo hakufanikiwa kutwaa taji la dunia, kuwa namba tatu
kwenye taji la mrembo mwenye malengo ambalo kuacha taji la dunia ili
linafuatia, Brigitte anahitaji kupongezwa," alisema.
Alisema
kuwa Brigitte ameonyesha ushujaa na kuwapita warembo kutoka mataifa
makubwa dunia ambao walichuana kwenye mashindano hayo na yeye kufanikiwa
kuingia hatua ya tatu bora kwenye taji hilo.
No comments :
Post a Comment