Mkurugenzi
wa Kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton ya Dar es Salaam Bw. Judd
Lehmann (kulia) akikabidhi moja ya taa ya Umeme Jua kwa mmoja wa
wanafunzi wa shule ya msingi Dihimba mkoani Mtwara. Anayeshuhudia tukio
hilo ni Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Serikali za Mitaa na Tawala
za Mikoa (Tamisemi) Mh. Hawa Ghasia (katikati).
Mkurugenzi
wa Mauzo wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Bw. Florenso Kirambata
akimkabidhi Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Serikali za Mitaa na
Tawala za Mikoa (Tamisemi) Mh. Hawa Ghasia (katikati) aina ya taa
zinazitumia Nishati ya Jua huku mtoto wa shule msingi Dihimba akishiriki
kupokea taa hiyo.
Waziri
wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa
(Tamisemi) Mh. Hawa Ghasia akimkabidhi taa ya Umeme Jua mmoja wa
wanafunzi wa shule ya msingi Dihimba.
Mkurugenzi
wa Mauzo wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Bw. Florenso Kirambata
akitoa mafunzo ya matumizi ya taa hizo kwa wanafunzi wa shule ya msingi
Dihimba mkoani Mtwara.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya msingi Dihimba wakati wa hafla ya kukabidhiwa
taa za Umeme wa Nishati mbadala zilizotolewa na Hoteli ya Double Tree.
Hoteli
ya Double Tree by Hilton ya jijini Dar es Salaam imeendelea na kampeni
zake kabambe ya matumizi ya nishati ya jua kwa kugawa taa 200 kwenye
shule ya Msingi Dihimba kata ya Dihimba wilaya ya Mtwara vijijini Mkoani
wa Mtwara, Moblog linaripoti.
Akizungumza
kwenye hafla hiyo fupi ya kugawa taa hizo, Waziri wa Nchi ofisi ya
Waziri Mkuu, Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (Tamisemi) Hawa Ghasia
amesema kwamba msaada huo wa Double Tree kwa shule hiyo ni kielelezo
tosha kwamba sekta binafsi zina mchango mkubwa katika sekta ya elimu
hapa nchini.
“Napenda
kuchukua fursa hii adhimu kuwashukuru uongozi na wafanyakazi wote wa
Double Tree kwa msaada wao mkubwa kwa shule yetu ya hapa Dihimba ambapo
watoto wetu watasoma katika mazingira rafiki yatayowawezesha kufaulu
mitihani yao,’ amesema Ghasia.
Waziri
Ghasia amesema kwamba kutokana na mabadiliko ya tabia nchi Serikali,
wananchi na wadau wote wa maendeleo hawawezi kuendelea kutegemea umeme
wa vyanzo vya maji na badala yake umeme wa jua ambao ni nishati mbadala
ni ufumbuzi wa tatizo la nishati nchini.
Amesema
mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya nchi hasa kwenye nishati
ni muhimu kwa sababu ni nishati ndio injini ya Uchumi wa taifa lolote
lile hapa duniani kwa sasa.
‘lakini
kampeni hizi zitakuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi kutambua na kuelewa
nishati mbadala na umuhimu wake katika maisha ya kila siku ikiwemo
mazingira,” alisisitiza
Hoteli
ya DoubleTree ilizindua rasmi kampeni ya matumizi ya nishati ya jua
ambayo itadumu kwa muda wa miaka miwili katika shule za msingi nchi
nzima miezi kadhaa iliyopita.
DoubleTree
itakuwa ikigawa taa 200 za mezani zenye kutumia nishati ya jua kwa
wanafunzi wa darasa la saba kwa shule tofauti kila mwezi, lengo likiwa
nikuwafanya wawe na ufahamu zaidi juu ya chanzo kingine cha umeme
ambacho ni rafiki wa mazingira kwa kupitia mafunzo katika madarasa yao.
Katika
kata ya Dihimba ina jumla ya wanafunzi wa shule za msingi wavulana 654
na wasichana 645 jumla yao ni 1299. Shule ya msingi Dihimba imepata
mafanikio ya kielimu kwa mwaka 2012/2013 kwa kushika nafasi ya nne kati
ya kata 28 katika mtihani wa taifa wa darasa la saba mwaka jana.
Katika
matokeo hayo shule ya msingi Dihimba ilishika nafasi ya nne kati ya
shule 98 kiwilaya na mafanikio mengine ni kuandikisha wavulana 135 na
wasichana 126 katika kujiunga na darasa la kwanza mwaka huu.
No comments :
Post a Comment