Klabu ya Manchester United imeweka wazi kwamba haitanunu tena mchezaji katika kipindi hiki cha usajili.
Rai hiyo imetolewa na kocha wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson akisema wamefikia kikomo cha biashara hivyo watu wanapaswa kusahau nani na nani walikuwa wakiwafuatilia na kuweka bayana kwamba mchezaji Michael Owen atakuwa akivaa jezi nambari saba.
Amesema wakati soko linapokuwa limepamba moto, wao huwa hawako tayari kufanya makkubaliano.
Wadau wengi wa soka walitaraji kuona dau la Pauni milioni 80 toka katika mauzo ya Cristiano Ronaldo ambaye ametua Real Madrid lakini imeonekana kwamba zimetumika robo tatu tu baada ya Owen, Antonio Valencia, Gabriel Obertan wakitumia jumla ya dau la pauni milioni 20.
Mzee Furgason amesema Valencia na Obertan wote ni wachezaji wenye umri mdogo, lakini ni wanauwezo mkubwa wa kusakata kandanda.
Ameongeza kuwa wako na mzee mmoja akimaanisha Owen. lakini amedai anauzoefu wa kutosha na anaamini atafunga magoli.
RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN ATOA MKONO WA EID KWA WENYE UHITAJI DODOMA
-
Mkuu Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule Machi 30,2025 amekabidhi kwa
niaba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia
Suh...
32 minutes ago
No comments :
Post a Comment