Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United ya Uingereza Quinton
Fortune, akipiga mpira kuashiria uzinduzi rasmi wa michuano ya vijana
wenye umri chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars. Uzinduzi huo
ulifanyika jana, Mei 10, kwenye Hoteli ya Sea Clif, jijini Dar es
Salaam.
Mchezaji wa zamani wa Manchester United ya Uingereza Quinton Fortunewa
pili kulia, akionyesha waandishi wa habari (hawako pichani) baadhi ya
vifaa vya michezo vitakavyotumika kwenye michuano ya soka ya kimataifa
kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars jana
kwenye Hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam. Kati ni Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Technologia Mh. Professa Makame Mbarawa, wa
kwanza kulia ni Mkurugenzi Mashindano wa TFF Sandy Kawembe, Mkurugenzi
Mtendaji wa Airtel Tanzania Sam Elangallor na Mkurugenzi Bidhaa Airtel
Afrika Obina Justine.
KAMPUNI ya Airtel Tanzania imezindua awamu ya pili ya mpango wa kuibua
na kusaka vipaji vya soka unaojulikana kama ‘Airtel Rising Stars’, zoezi
lililoendeshwa na nyota wa zamani wa Manchester United, Quinton
Fortune.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam,
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sam Elangallor, alisema
mafanikio ya mwaka jana yanaonyesha mpira wa miguu, una uwezo wa
kuunganisha makabila mbalimbali na pia kuleta hamasa kwa jamii, kuanzia
ngazi ya chini hadi taifa.
Alisema mwaka jana zaidi ya timu 11,000 Afrika, zilijiandikisha
kushiriki kwenye michuano hiyo, kuanzia kwenye mtoano na kuchagua
wachezaji ambao waliunda timu zilizoshiriki kwenye ngazi ya mkoa.
“Awamu hii ya pili, inafuatia ile ya kwanza ya mwaka jana kuwa na
mafanikio makubwa. Lengo la mpango huu ni kuvipa vipaji vinavyochipukia
chini ya umri wa miaka 17, nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kwa makocha
waliobobea na pia kupata nafasi ya kuendeleza vipaji vyao,” alisema.
Alisema kama ilivyokuwa kwa mwaka jana, mpango huu utaanzia ngazi ya
mkoa, taifa na kufuatiwa na kliniki ya soka ya kimataifa chini ya
wakufunzi kutoka klabu ya Manchester United ya Uingereza.
Aliongeza kuwa mwaka huu kutakuwa na mashindano ya siku nne ya timu
bingwa kutoka kila nchi itakayoshiriki michuano hiyo, kushindania taji
jipya la Airtel Rising Stars African Champion.
“Tumeamua kuongeza mshindano ya nchi na nchi mwaka huu, kwa nia ya
kuweza kuwafanya vijana kushirikiana na kuwaleta karibu kwa kupitia njia
ya pamoja, ambayo ni mchezo wa kandanda. Tunaamini ya kwamba michuano
hii italeta hamasa na umoja kwa wachezaji,” alisema.
Kwa mwaka huu, michuano hii imezinduliwa na mchezaji wa zamani wa
Manchester United, Quinton Fortune, ambaye alisajiliwa na Sir Alex
Ferguson mwaka 1999, akitokea Atletico Madrid, wakati huo akiimarisha
timu yake kushinda matajizaiti tembelea
http://mamapipiro.blogspot.com/
No comments :
Post a Comment