MBUNGE
wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari (Pichani) ametii amri ya polisi
baada ya kuibuka na kujisalimisha leo makao makuu ya polisi mkoa wa
Arusha kufuatia agizo la jeshi hilo lililotolewa jana na mkuu wa kitengo
cha ufuatiliaji na tathimini Naibu kamishna wa polisi Issaya Mngulu la
kumtaka mbunge huyo kujisalimisha kutokana na maneno yake ya uchochezi.
Nassari
alijisalimisha kituoni hapo majira ya saa tano asubuhi na kasha
kulazimika kuondoka kituoni hapo baada ya kuwakosa kaimu kamanda wa
polisi mkoani Arusha Akili Mpwapwa pamoja na Naibu kamishna Issaya
Mngulu waliokua wakihudhuria kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya
mkoa.
Mara baada ya kuondoka kituoni hapo Nassari alirejea tena kituoni hapo baada ya nusu saa akiwa na wakili wake Albart Msando
ambapo alipokelewa na kaimu kamanda na kasha kukutanishwa na Issaya
Mngulu na viongozi wengine wa polisi mkoa tayari kwa mahojiano.
Kwa
upande wake Nassari alipoulizwa kwanini alikaidi kutii amri ya polisi
iliyomtaka kufika kituoni kwa mahojiano alisema hakupata taarifa hizo
bali taarifa alizozipata za polisi ni kutoka kwa aliyekua kamanda wa
polisi mkoa wa Arusha Thobias Andengenye kupitia kwa ofisa mmoja wa
polisi kuwa alimuhitaji kufika kituoni hapo kwaajili ya kuagana baada ya
kamanda huyo kupata uhamisho kwenda jijini Dar es salaa kikazi.
Mahojiano
hayo ambayo mpaka tunakwenda mitamboni yalikua yakiendelea kwa zaidi ya
saa sita mpaka saa 11 jioni Nassari alikua akiendelea kuhojiwa
kuhusiana na tuhuma hizo zinazomkabili ikiwemo za kutoa kauli za
uchochezi katika mkutano wa hadhara uliofanyika siku ya jumamosi
iliyopita katika uwanja wa NMC Unga Ltd mjini Arusha.
Hata
hivyo muda wote akiwa anaendelea na mahojiano aliyekua mbunge wa Arusha
mjini Godbles Leman a wafuasi wengine wa Chadema walionekana nje ya
viwanja vya makao hayo makuu ya polisi ambapo hata hivyo baada ya muda
waliondoka pasipokujilikana walikoelekea.
Kwa
mujibu wa Kamishna Mngulu hapo jana a.lipozungumza na vyombo vya habari
alidai kuwa Nassari alisikika akitamka maneno hayo ya uchochezi kwa
kulipa jeshi la polisi siku tatu kuwapata waliosababisha kifo cha
aliyekua mwenyekiti wa Chadema kata ya Usa River wilayani Arumeru
Msafiri Mbwambo la si hivyo Rais Kikwete pamoja na Waziri Mkuu Pinda
wasikanyage Arusha.
Pia
alisema mara baada ya kauli hiyo Nassari alijitangaza kuwa yeye ndiye
Rais wa Arusha huku akimtangaza aliyekua mbunge wa Arusha mjini Godbles
Lema kuwa waziri mkuu.
Mngulu
alisema kauli nyingine ni ile ya kutangaza kuiunganisha mikoa ya kanda
ya kaskazini na ile ya kanda ya ziwa kuwa nchi inayojitegemea yaani
kujitangazia jamuhuri yake binafsi kama ilivyotokea Sudan Kusini.
Pia
alisema kauli nyingine ni ile iliyomuhusu motto wa Rais Kikwete
Ridhiwana Kikwete kwamba ana marafiki zake wa kike na kazi yake ni
kuwatambulisha kwa baba yake ili awateue katika nafasi mbalimbali za
uongozi na kwamba Rais Kikwete anateua viongozi kwa kushauriwa na
Ridhiwan.
Kauli
nyingine ni ile ya kutafuta vijana wapatao 500 ili kufanya maandamano
hadi ikulu ya magogoni jijini Dar es salaam kutokana na nchi hii
kutafunwa na wajanja huku Rais Kikwete akiangalia tuu.
Mbali
na ,mbunge huyo kuhojiwa viongozi wengine watatu wakiwemo na wanachama
wa chama hicho walihojiwa hapo jana kwa tuhuma hizohizo akiwemo
mwenyekiti wa baraza la vijana wa Chadema taifa John Heche,aliyekua
mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arusha Ally Bananga aliyehamia Chadema
hivi karibuni na aliyekua diwani wa kata ya Sombetini CCM Mawazo
Alphonce aliyehamia Chadema hivi karibuni.
Hata
kamishna Mngulu alisema mara baada ya mahojiano hayo jeshi lake
litaandaa jalada la kesi la kuliwasilisha kwa mwanasheria mkuu wa
serikali ili kuipitia na kuona iwapo kuna kesi ya kujibu au laa na kama
ipo watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao.
No comments :
Post a Comment