SHIRIKISHO
la ngumi la Kimataifa (IBF) limemteua Rais wa Shirikisho hilo katika
bara la Africa, Onesmo Alfred Ngowi kusimamia pambano la ubingwa wa
mabara linalotambuliwa na IBF.
Mpambano
huo utafanyika katika jiji la Accra nchini Ghana tarehe 26 Mei kati ya
bingwa wa mabara wa IBF Emmanuel Tagoe wa Ghana na mpinzani wake Antonio
De Vitis wa Italy katika uzito wa Junior Lightweight.
Katika
mpambano huo wa kutetea mkanda wa ubingwa wa IBF ambao unashikiliwa na
Emmanuel Tagoe wa Ghana Ngowi atasaidiwa na waamuzi wengine kama
ifuatavyo: Refarii: Roger Barnor (Ghana). Majaji: Francisco de Ruvo,
(Italy), Andre Pasquier (France) na Shadrack Acquaye (Ghana).
Mpambano huo uliopewa jina la “NI Sasa au Hakuna Tena”
bondia Joseph Agbeko wa Ghana atagombea mkanda wa dunia wa
Organizesheni ya Ngumi ya Kimataifa (IBO) akichuana na bondia Michael
Domingo wa Ufilipino katika uzito wa Bantam.
Bondia Josepgh Agbeko anayeishi katika mji wa Bronx katika jiji la New York
nchini Marekani atakumbukwa kwenye mpambano wake mkali wa kugombea
ubingwa wa IBF kati katika uzito wa Bantam kati yake na bondia Abner
Mares wa Mexico tarehe 3 mwezi Augusti 2011 katika jiji la Las Vegas,
Nevada nchini Marekani ambako ilibidi warudiane mara ya pili baada
yakutokea malalamiko ya kuonewa kwa Agbeko.
Hata
hivyo bondia Abner Mares alimshinda tena Joseph Agbeko waliporudiana
tarehe 18 November 2011 katika jiji la California, nchini Marekani.
Naye
bondia Joshua Okine wa Ghana ambaye alikuwa bingwa wa mabara wa IBF
katika uzito wa Middle kabla ya kupoteza ubingwa wake kwa kupandisha
uzito atapambana na bondia Theofiilus Teteh pia wa Ghana kugombea mkanda
wa WBO Africa.
Bondia Sammuel Amaoko a.k.a Bruno wa Ghana atapambana na bondia Sidney Siqueira wa Beazil kugombea mkanda wa WBO Africa katika uzito wa Heavyweight.
Mapambano haya yaliyoandaliwa na GoldenMike Boxing Promotions ya Ghana yatafanyika katika uwanja wa kimataifa wa El-Wak,jijini Accra nchini Ghana chini ya usimamiziwa Mamlaka ya Ngumi zaKulipwa ya Ghana (Ghana Boxing Authority, GBA)
Usimamizi wa Ngowi katika mpambano huu unakuja kipindi kifupi baada ya Francis Cheka wa Tanzania kuunyakua mkanda wa IBF Continental Africa Title katika uzito wa Super Middle tarehe 28 April mwaka huu!
Imetolewa na,
Onesmo A.M.Ngowi
No comments :
Post a Comment