Timu
ya Azam Fc leo imelambishwa maji ya miwa na Mtibwa Sugar katika mchezo
uliokuwa wa marudiano baada ya ule uliovuvjika wiki iliyopita katika
Uwanja wa Chamazi, ambapo Mtibwa Suga wameibuka Kidedea kwa kuwachabanga
mabao 2-1 na kupoteza matumaini ya Azam Fc kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu
ya Vodacom 2012. Babao wa Mtibwa Sugar yamefungwa na Waziri Ally na la
pili likitupiwa na Juma Abdul, huku bao la Azam Fc likiwekwa kimiani na
John Boko. Kwa matokeo hayo sasa Simba imejikatika tiketi ya kutwaa
Ubingwa bila ya mpinzani, huku wakisubiri kumalizia mchezo wao wa mwisho
katika msimu huu wa Ligi Kuu na Mahasimu wao wa Jadi Yanga, mchezo
unaotarajia kupigwa siku ya Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini dar
es Salaam.
DKT.NCHIMBI KUMUWAKIILISHA RAIS MAZISHI YA BI SUZANA MAGUFULI
-
Makamu wa Rais, akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu,Bi
Suzana Magufuli, Kilimani Chato, pamoja na kuwafariji wafiwa kufuatia
msiba...
2 days ago

No comments :
Post a Comment