Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar imeelezea malengo yake iliojiwekea katika kuimarisha Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara, Anga,Bandari pamoja na Mawasiliano.
Ukizungumza katika Kikao Maalum na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohd Shein huko Ikulu jana Uongozi wa Wizara hiyo umesema kuwa unatarajia kujenga Miundombinu Bora na endelevu ya Barabara ili kushajiisha Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii Nchini.
Wamesema kuwa katika Azma hiyo Miradi mbali mbali ya Barabara Kuu za Unguja na Pemba pamoja na zile za Vijijini zikiwemo Amani-Mtoni,Mgagadu-Kiwani,Ole-Kengeja zitatekezwa pamoja na kuandaa Sera na Sheria ya Matumizi ya ICT na kuilimisha Jamii umuhimu wa kuhifadhi Miundombinu hiyo.
Walisema kuwa Wizara ya Miundombinu inatarajia kutekeleza Miradi ya Miundombinu ya Viwanja vya Ndege Unguja na Pemba ikiwemo Maegesho na Njia za kupitia Ndege katika Uwanja wa Abeid Amani Karume na Jengo Jipya la Abiria.
Wakimuelezea Rais juu ya Shirika la Bandari Zanzibar wamesema kuwa Wanatarajia kuzifanyia matengenezo Gati za Kisiwani Pemba,Kuengeza eneo kwa ajili ya kuweka Makontena katika Bandari ya Malindi Zanzibar pamoja na kulitafutia ufumbuzi suala la Mnara wa kuongozea Meli uliopo Nungwi.
Nae Dk Shein ameipongeza Wizara hiyo kwa Kujipangia Malengo yake ilijiwekea katika Bajeti yake ya mwaka wa Fedha 2011/2012 na kusisitiza kuwa kila Idara,Shirika na Taasisi ya Wizara hiyo kuwajibika ipasavyo ili kufikia lengo walilojiwekea.
Amesema kuwa upo umuhimu wakuimarisha Karakana ya Serikali iliopo Chumbuni kutokana na umuhimu wake Mkubwa katika ukusanyaji wa Mapato pamoja na Matengenezoya Gari za Serikali.
Dk Shein hii ni Wizara ya nane kukutana nayo kati ya Wizara kuminasita za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika mfululizo wake wakukutana na Wizara zote kusikiliza Malengo waliojiwekea katika Bajeti ya Fedha kwa mwaka 2011-2012.
No comments :
Post a Comment