Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, August 13, 2011

Mitambo ya Umeme ya Aggreko Yawasili Nchini





















Mitambo ya Aggreko ikishushwa, tayari kwa kufungwa.


Sehemu ya mitambo ya umeme ya Aggreko ikishushwa Ubungo jijini Dar es Salaam tayari kuanza kufungwa na umeme wake kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa.


Moja ya kontena lenye mitambo ya Aggreco likiwasili leo mchana ubungo jijini Dar es Salaam


Meneja wa Mahusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Badra Masood, akizungumza na waandishi wa habari leo mchana kwenye mitambo ya kufua umeme, Ubungo jijini Dar es Salaam. Badra alisema kuwa magao wa umeme utakoma kufikia mwezi Disemba mwaka huu. Akielezea mikakati mbali mbali ambayo TANESCO imefanya ni alisema kuwa ni pamoja na kukodisha mitambo yenye uwezo w kuzalisha Megawati 100, kutoka Kampuni ya Aggreco ya Mombasa, Kenya. Mitambo iliyowasili leo na kazi ya kuifunga itatarajiwa kuanza hivi hivi karibuni. Akielezea zaidi kuhusu ujio wa mitambo hiyo ya Aggreco, Badra alisema kuwa hii ilikuwa ahadi ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alipokuwa akiwasilisha bajei ya wizara yake Bungeni hivi karibuni. Mipango mingine ya kumaliza mgao wa umeme ifikapo Disemba mwaka huu ni pamoja na kutumia mitambo ya Symbion yenye uwezo wa kuzalisha Megawati 112, na mitambo ya Jacobsen inayoendelea kufungwa hatua inayoipa Tanesco uhakika wa kumaliza kero ya mgao wa umeme mwezi Disemba mwaka huu.Picha na Victor Makinda




No comments :

Post a Comment