Pambano hilo ambalo litakuwa la raundi nane litasindikizwa na burudani kutoka katika kundi la 'Makhirikhiri wa bongo' huku likitanguliwa na mapambano manne ya utangulizi ambapo yatafanyika katika ukumbi wa CCM Mwinjuma wa Mwananyamala Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa pambano hilo Ibrahim Kamwe 'Bigright' alisema maandalizi ya pambano hilo yamekamilika na kuwataka wadau wa mchezo wa ngumi kuweza kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia mapambano hayo.
Bigright aliyataja ambambano ya utangulizi ni kati ya Anthon Mathias na Shabani Madilu ambapo pambano lao litakuwa la raundi sita.
Wengine ni Joseph Mbowe na Ezekiel Ezekiel raundi nne, Isa Omari na Kade Hamis raundi sita na Sadat Miyeyusho na Herman Richard raundi sita.
Pia wamo Yona Miyeyusho na Haruna Said raundi nne, Martine Richard na Jumanne Kilumbelumbe raundi nne na pambano la mwisho litakuwa kati ya Mwaite Juma na Franck Pury raundi nne.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na huzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kibao.
DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha maarufu Rajabu Mhamila 'SUPER D BOXING COACH' hapo
na kwa Dar es Salaam DVD hizo zinapatikana katika Makutano ya Barabara ya Uhuru na Msimbazi
DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha maarufu Rajabu Mhamila 'SUPER D BOXING COACH' hapo
na kwa Dar es Salaam DVD hizo zinapatikana katika Makutano ya Barabara ya Uhuru na Msimbazi
No comments :
Post a Comment