Meneja mahusiano mwandamizi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Noves Moses (kushoto)
akimkabidhi jezi nahodha wa timu ya netiboli ya waandishi wa habari za
michezo nchini (Taswa Queens) Imani Makongoro (Kulia) katika halfa fupi iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jana. Katikati ni Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary . Picha/Mpigapicha wetu
*****************************************
Na Mwandishi Wetu, Dar
Benki ya Posta Tanzania (TPB) imeendelea kuisadia timu ya Waandishi wa habari za michezo
nchini (Taswa SC) baada ya kuikabidhi vifaa vya michezo kwa ajili ya
kutumika katika mashindani na michezo mbali mbali ya kirafiki.
Benki
hiyo imekabidhi seti za jezi kwa timu hizo zikiwa na jumla ya thamani
ya Sh1,180,000 kwa timu ya mpira wa miguu maarufu kwa jina la Taswa FC
na timu ya netiboli ambayo pia inajulikana kwa jina la Taswa Queens.
Akizungumza
katika makabidhiano hayo, Meneja mahusiano mwandamizi wa Benki ya Posta
Tanzania (TPB) Noves Moses alisema kuwa msaada huo ni sehemu ya
shughuli za benki kijamii na kutambua mchango mkubwa wa waandidshi wa
habari hapa nchini.
“Waandishi
wa habari wameonyesha mfano mkubwa kwa kucheza soka na netiboli, pia
niliona mnafanya mazoezi ya ngumi chini ya bondia Thomas Mashali, huu ni
mfano wa kuigwa na ndiyo maana tumevutiwa na utendaji na maendeleo
yenu,” alisema Noves.
Mwenyekiti
wa Taswa SC, Majuto Omary aliishukuru TPB kwa kuendelea kuwakumbuka na
kuahidi kutumia jezi hizo kwa kushinda mechi na wala si kutoka sare au
kufungwa.
“Tunajivunia
uwepo wa Benki ya Posta kwa kuthibitisha kuwa ni benki halisi ya
Watanzania, nachukua fursa hii kuwaomba Watanzania kufungua akaunti zao
katika benki hii na vile vile kuomba wadau wengine kufuata mfano wao kwa
kuisaidia Taswa SC ili iweze kufanikisha ziara zake,” alisema Majuto.
No comments :
Post a Comment