
Sehemu
 ya Mabaki Lori la mafuta lililoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo 
mara baada ya kupiga mweleka likiwa katika hatakati ya kulikwepa gari 
lingine lililokuwa likitokea Kongowe ambalo liliingia ghafla barabarani 
bila ya tahadhari,hali iliyolipelekea Lori hilo kukosa mwelekeo na 
kupiga mweleka.
Lori 
hilo pamoja na kupiga kwake mweleka halikuwa na madhara yeyote wala 
dalili ya kusema litawaka moto.Baada ya muda likaja kundi la vijana 
likiwa na madumu na mifuko ya plastiki na kuanza kuchukua mafura 
yaliyokuwemo kwenye lori hilo hali iliyopelekea kutokea mlipuko mkubwa 
ulioliteketeza lori hilo.
haijafahamika
 mpaka sasa kama kuna mtu yeyote aliepoteza maisha katika moto huo,ila 
hasara kubwa imeonekana kutokea kwa nyumba tatu zilikuwepo jirani na 
eneo la tukio zimeteketea kwa moto,ambazo moja ni ya makazi ya watu,duka
 la juma la Mchele pamoja nyumba ya kulala wageni.

Sehemu ya Lori hilo likiwa limeteketea kabisa.

Sehemu ya Wakazi wa Maeneo hayo wakiangalia kilichotokea huku wakiwa hawaamini wanachokiona.

Sehemu ya Nyumba zilizoteketea kwa moto.
PICHA KWA HISANI YA MTAA KWA MTAA BLOG
No comments :
Post a Comment