-Viongozi
 wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakionesha hati za waraka 
walizotiliana saini za ushirikiano katika viwanja vya Jangwani Dar es 
Salaam leo. Kutoka kulia ni, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), 
Maalimu Seif Sharifu Hamad , Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na 
Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba 
na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
 Waendesha bodaboda ambao ni wafuasi wa Ukawa wakiingia kwa maandamano katika viwanja vya Jangwani.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalimu Seif Sharifu Hamad , akihutubia kwenye mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Emanuel Makaidi akihutubia kwenye hafla hiyo kabla ya kutiliana saini waraka wa ushirikiano.
 Makatibu
 wakuu wa vyama vinavyuunda Ukawa, wakionesha ishara ya mshikamano baada
 ya kusaini waraka huo wa ushirikiano. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa 
Chama cha NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. 
Willibrord Slaa, Katibu Mkuu wa CUF, Maalimu, Seif Sharifu Hamad na 
Katibu Mkuu wa Chama NLD, Tozi Matwange.
 Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
 Mwanasheria
 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Tundu Lisu (kulia), akimkaribisha
 Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chama cha Wananchi (CUF), Ismail Jusa 
Ladhu, kuzungumza katika mkutano huo.
 Wafuasi wa ukawa wakionesha vidole vitatu juu wakimaanisha kuikubali serekali tatu inayotakiwa na Ukawa.
 Wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF), wakiwa 
kwenye mkutano huo.
Vijana wa
 chama cha chadema wakiwa juu ya gari wakifuatilia matukio mbalimba 
yaliyokuwa yakiendelea uwanjani hapo. Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com
No comments :
Post a Comment