Msanii
 wa muziki wa kizazi kipya miondoko ya Hip Hop, Rashid Makwiro, ‘Chidi 
Benzi’ akisindikizwa na askari Polisi wakati akiwasili katika chumba cha
 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo, kujibu 
mashtaka matatu likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya kwenye Uwanja wa 
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, hivi 
karibuni. 
**************************************
Msanii
 wa muziki wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chid Benzi’ leo amepandishwa 
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka matatu 
likiwemo la matumizi ya dawa za kulevya.
Chid
 Benzi, alipandishwa kizimbani majira ya saa nane mchana, mbele ya 
Hakimu Warialwande Lema, ambaye alimtaka msanii huyo atolewe nje 
kutokana na uvaaji mbaya wa suruali yake kwani alivaa ‘Kata kei’ ili 
avae vizuri nguo.
Akisomewa
 mashitaka yake, na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono, alidai 
kwamba mnamo 24 Oktoba 2014, Chidi Benzi alikutwa na dawa hizo kwenye 
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Alidai
 kwamba, shitaka la kwanza linalomkabili ni kukutwa na madawa ya kulevya
 aina ya Heroin yenye thamani ya sh.38, 638. Pia shitaka la pili ni 
kukutwa na gramu 1.72 za dawa kulevya aina ya Bangi yenye thamani 1,720.
Mbali
 na hilo, shitaka la tatu ni kukutwa na vifaa vinavyotumika kuvutia dawa
 hizo za kulevya, ambapo alikutwa na Kifuu cha nazi kitupu na kijiko 
kimoja.
Hata
 hivyo, wakili huyo alidai kwamba upelelezi wa shauri hilo bado 
haujakamilika. Hakimu Lema alihairisha kesi hiyo hadi Novemba 11, mwaka 
huu baada wadhamini kushindwa kujitokeza kwa haraka.
Hakimu Lema alisema, mshitakiwa huyo anatakiwa kudhaminiwa na wadhamini wawili wa kudumu pamoja na bonfdi ya Sh.milioni 1.
Hali
 hiyo ya kushindwa kupata dhamana ilizua hali ya simanzi kwa familia 
yake, kutokana na kuchelewa kujitokeza kwa wadhamini wake mbele ya 
Hakimu na hivyo kushindwa kupata dhamana.
Chidi
 Benzi alikamatwa na dawa za kulevya katika hatua ya ukaguzi kwaajili ya
 kupanda ndege ya Fastjet akielekea jijini Mbeya, juzi jioni katika 
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Msanii wa Hip Hop, Rshid Makwiro ‘Chidi Benzi’ akiingia Mahakamani leo.
Chidi Benzi akipanda karandinga kwa ajili ya kuelekea katika mahabusu ya Segerea.
No comments :
Post a Comment