Mechi
 ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Yanga 
na Simba iliyochezwa juzi (Oktoba 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es 
Salaam imeingiza sh. 427,271,000.
Washabiki
 49,542 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa 
sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Asilimia 18 ya Kodi ya 
Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 65,176,932 wakati asilimia 5
 ya gharama ya tiketi kwa CRDB ni sh. 21,363,550.
Kwa
 upande wa Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) ambayo ni sh. 
1,000 kwa kila tiketi, timu mwenyeji Yanga imepata sh. 17,339,700, Chama
 cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 7,431,300 na 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 24,771,000.
Mgawo
 mwingine wa mapato hayo ni Uwanja sh. 43,678,277.67, gharama za mchezo 
sh. 24,751,024.01, Bodi ya Ligi sh. 23,295,081.42, TFF sh. 
17,471,311.07, DRFA sh. 10,191,598.12, timu mwenyeji Yanga sh. 
100,460,038.64 na timu ngeni Simba sh. 71,341,186.86.



No comments :
Post a Comment