Meneja
 masoko wa kinywaji cha GrandMalt Tanzania Fimbo Buttala akizungumza na 
waandishi wa habari katika ukumbi wa Kebbys Hotel juu ya uzinduzi wa 
Tamasha la Filamu jijini Tanga kuanzaia jumamosi ya Tarehe 04/10/2014 
hadi 08/10/2014 kushoto ni Sinle Mtambalike, Ray Kigosi na kulia ni Rose
 Ndauka,Shamsa Ford.
Msanii
 Rose ndauka akizungumza na waandishi wa habari juu ya ushiriki wao 
kwenye tamasha kubwa la filamu litakalofanyika jijini Tanga jumamosi ya 
wiki hii na kuwashirikisha wasanii wote wa kundi la Bongo Muvie kuliani 
shamsa ford na wasanii wengine
Msanii Single Mtambalike.
Meneja masoko wa kinywaji cha GrandMalt Tanzania Fimbo Buttala akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Kebbys Hotel juu ya uzinduzi wa Tamasha la Filamu jijini Tanga kuanzaia jumamosi ya Tarehe 04/10/2014 hadi 08/10/2014 kushoto ni Sinle Mtambalike, Ray Kigosi na kulia ni Rose Ndauka,Shamsa Ford
NA BONGOWEEKEND REPORTER
TAMASHA
 la wazi la filamu Tanzania “Grand Malt Film Festival 2014” sasa 
litafanyika kuanzia Oktoba 4hadi 8 mwaka huu kwenye viwanja vya 
Tangamano jijinia Tanga imeelezwa.
Akizungumza
 jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania 
(TBL), Fimbo Butallah, alisema kuwa maandalizi ya tamasha hili 
yamekamilisha na uzinduzi rasmi utafanyika Jumamosi Oktoba 4 na mgeni 
rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Halima Dendegu.
Butallah
 alisema kuwa tamasha hilo ni la wazi na hakuna kiingilio kwa wadau wa 
Sanaa hiyo ya filamu na uzinduzi utafanyika kuanzia saa tisa mchana.
Alisema
 kuwa kabla ya uzinduzi wa tamasha hilo, wasanii mbalimbali nyota ambao 
wanatarajia kushirikishi tamasha hilo watafanya kazi ya jamii kwa 
kutembelea kituo cha watoto wenye matatizo ya ngozi.
Aliongeza
 kuwa kupitia tamasha hili Grand Malt inasaidia kuinua na kutangaza kazi
 za wasanii wa hapa nchini na kuwapa nafasi ya kuwakutanisha na wadau na
 mashabiki wao.
Naye
 Kaimu Mwenyekiti wa Bongo Movie, Single Mtambalike, aliishukuru Grand 
Malt, kwa kufanikisha tamasha hili kwa mwaka wa tatu mfululizo.
Mtambalike
 alisema kuwa Sanaa ya filamu inasaidia kuwapatia ajira watu mbalimbali 
hapa nchini na kutaja katika maandalizi ya filamu moja, Zaidi ya wasanii
 50 wanatumika kucheza filamu hiyo.
“Tunaashukuru
 sana Grand Malt na Sophia Records kwa kufanikisha tamasha hili ambalo 
linathibitisha wazi kuwa tasnia hii ni biashara kubwa”, alisema 
Mtambalike.
Rose
 Ndauka, ambaye naye ni msanii ya filamu aliwataka wadau wote kujitokeza
 na kutaja moja ya vitu watakavyotoa kwa watoto watakaowatembelea ni 
magodoro 60.
Awali tamasha hilo lilipangwa kufanyika mapema mwezi Agosti mwaka huu mkoani Mtwara.
No comments :
Post a Comment