
Rais 
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi jengo la kitega 
uchumi la mfuko wa pensheni la PPF mjini Mwanza jana jioni.Wengine 
katika picha kutoka kushoto,ni Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli,
 Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana Wiliam Erio, Naibu Waziri wa Fedha Mhe. 
Adam Malima, Mwenyekiti wa Bodi ya PPF Bwana Ramadhani Kija, na Mkuu wa 
Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evaristi Ndikilo.

Jengo 
la Kitega uchumi la mfuko wa pensheni wa PPF lililozinduliwa rasmi na 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mjini Mwanza jana jioni.

Rais 
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana William Erio 
wakiangalia madhari nzuri ya jiji la Mwanza wakiwa katika jengo jipya la
 kitega uchumi la mfuko wa pensheni wa PPF muda mfupi baada ya 
kulizindua mjini Mwanza jana jioni.
Naibu 
Waziri wa Fedha Adam Malima, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PPF 
Bwana Ramadhani Kija(watatu kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana 
William Erio(kulia) wakimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete 
kuzindua jengo la kitega uchumi la PPF mjini Mwanza jana jioni.
Mkurugenzi
 Mkuu wa PPF Bwana William Erio akitoa maelezo kwa Rais Dkt.Jakaya 
Mrisho Kikwete ndani ya mgahawa uliopo katika jengo jipya la kitega 
uchumi la PPF muda mfupi baada ya kulizindua rasmi mjini Mwanza.Kushoto 
ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo.
Rais 
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na viongozi na wafanyakazi wa Shirika
 la PPF baada ya kuwa amezindua Jengo la Kitega Uchumi la Shirika hilo 
katikati ya Jiji la Mwanza jana, Ijumaa, Oktoba 10, 2014. Rais Kikwete 
yuko katika ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani Mwanza.(picha na Freddy 
Maro)
No comments :
Post a Comment