
Pichani ni 
mti unaodaiwa kunyanyuka ghafla baada ya kuanguka miaka mitatu 
iliyopitakatika kijiji cha Mfuto kata ya Ufuluma ,ambapo wilaya ya Uyuwi
 mkoani Tabora.
Katika 
hali ya kushangaza huku kila mtu akifikiria yake baaya ya juzi huko  
mkoani  Tabora, kutokea tukio la aina yake ambapo inaelezwa kuwa mti  
aina ya Msufi uliokuwa  umeanguka yapata miaka  mitatu  iliyopita 
umesimama  ghafla  tena  kwa  sauti  kubwa ya  mrindimo na kuwafanya 
wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo.
Tukio hilo limetokea  Oktoba 17,mwaka huu,katika kijiji cha Mfuto kata ya Ufuluma katika wilaya ya Uyuwi mkoani Tabora.
Inaelezwa kuwa mti huo wenye kipenyo cha futi 2 uliinuka na kuwa kama zamani baada ya kutokea upepo mkali katika kijiji hicho.
Wananchi walikusanyika kila  mmoja akitaka kuchukua angalau gome la 
mti huo  kwa ajili ya  dawa ama kumbukumbu , na haya  ndio maajabu ya 
Tanzania.
No comments :
Post a Comment