Meneja
 Masoko, Mawasiliano na Elimu kwa Umma kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi
 na Udhamini (RITA) Bw. Josephat Kimaro akiwaeleza  waandishi wa habari 
(hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu kueneza Mkakati  wa 
Usajili na Kutoa Vyeti vya Kuzaliwa kwa Wanafunzi wa Manispaa ya 
Kinondoni na Temeke baada ya kumaliza Manispaa ya Ilala. Kulia ni Afisa 
Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bi Fatma Salum.
Baadhi
 ya waandishi wa habari wakisikiliza taarifa ya mafanikio kutoka kwa 
 Meneja Masoko, Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa Wakala wa Usajili, 
Ufilisi na Udhamini (RITA) Bw. Josephat Kimaro leo jijini Dar es Salaam.
 Picha na MAELEZO.
**********************
Na Fatma Salum- Maelezo
Jumla
 ya wanafunzi 15,120 wa shule za Msingi na Sekondari katika Manispaa ya 
Ilala jijini Dar es Salaam wameweza kusajiliwa na kupata vyeti vya 
kuzaliwa kupitia Mkakati wa Usajili na Kutoa Vyeti vya Kuzaliwa 
unaotekelezwa na Wakala wa Usajili,Ufilisi na Udhamini (RITA).
Hayo
 yamesemwa na  Meneja Masoko, Mawasiliano na Elimu kwa Umma kutoka 
Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Bw. Josephat Kimaro wakati
 wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
“Mkakati
 huu umeonesha mafanikio makubwa kwani mpaka sasa wanafunzi  15,120 
wamepata vyeti vya kuzaliwa wakiwemo wasichana 7,712 na wavulana 7,408 
kutoka shule 201 za Manispaa ya Ilala ambapo 201 ni shule za Msingi na 
96 ni Sekondari.” Alisema Kimaro.
Akifafanua
 zaidi kuhusu mkakati huo uliozinduliwa mwezi Aprili mwaka huu Kimaro 
alisema umelenga kusogeza huduma karibu na wananchi kwa kuwapatia 
wanafunzi vyeti vya kuzaliwa wakiwa shuleni badala ya wazazi kuvifuata 
kwenye Ofisi za RITA.
Aidha
  umesaidia kuongeza uelewa kwa wanafunzi, wazazi na walezi kuhusu 
umuhimu wa cheti cha kuzaliwa kwani wazazi wengi wameshawishika kufanya 
usajili na kupata vyeti kwa ajili ya familia nzima.
Pia
 Kimaro aliongeza kuwa baada ya mkakati huo kufanikiwa katika Manispaa 
ya Ilala RITA inatarajia kuendeleza katika Manispaa za Temeke na 
Kinondoni mnamo mwezi  Januari 2015 zikifuatiwa na Manispaa nyingine za 
Tanzania Bara.
Akitoa
 wito kwa wazazi na walezi Kimaro amewataka kutumia fursa hiyo kuwapatia
 vyeti watoto wao wanaosoma katika shule ambazo program inatekelezwa 
kwani hutumia mfumo rahisi kwa  gharama nafuu na mtoto hupata cheti 
halisi.


No comments :
Post a Comment