Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, October 2, 2014

IPTL YAIMWAGIA TASWA MILIONI 20 KUANDAA TUZO ZA WANAMICHEZO.


Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Harbinder Sigh Seth (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 20 kwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto (wapili kulia) ikiwa ni mchango wa IPTL kusaidia maandalizi ya Tuzo za wanamichezo bora nchini. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni ni Makamu Mweyekiti wa TASWA, Egbert Mkoko, Katibu Mkuu, Amir Mhando na Mwanasheria na Mshauri Mkuu wa IPTL,Joseph Makandege na kulia ni Mjumbe wa TASWA, Rehure Richard Nyaulawa

 Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Harbinder Sigh Seth akiwaeleza wanahabari furaha yake ya kuisaidia TASWA kitita hicho cha fedha kusaidia wanamichezo ambapo nae alikiri kuwa ni miongoni mwa wanamichezo na amewahi kuwa Mshindi wa tatu wa Mbio za Magari Afrika.
 Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Harbinder Sigh Seth (katikati) akiwaongoza wanahabari kuangalia mitambo ya Kampuni hiyo ambayo inazalisha umeme. Kulia ni Katibu mkuu wa TASWA, Amir Mhando na Kushoto ni Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto.
Waandishi wa habari wakiingia kuangalia uzalishaji wa umeme katika mitambo ya IPTL.
Picha na Mroki mroki

No comments :

Post a Comment