GODFREY NZOWA(Kamishina msaidizi Mwandamizi kitengo cha kudhibiti na 
kupambana na Dawa za kulevya) akionyesha baadhi ya madawa yaliyokamatwa.
 
kuwakamata na kilo saba za Dawa za Kulevya aina ya 
Heroin,zinazodhaniwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 300 
usiku wa kuamkia Jumanne hii.
Watu hao wamekamatwa maeneo ya Magomeni jijini Dar es Salaam,usiku wa kuamkia Jumanne hii.
Wafanyabiashara wanaoshikiliwa na Kitengo hicho ni Mwalami Mohamed 
Chonji,Mariki Zuberi,Taka Adam,Rehan Musso na Abdul Abdallah ambao 
wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Kamishina msaidizi Mwandamizi wa Kitengo hicho,Godfrey Nzowa 
amesema,kukamatwa kwa watu hao kunafuatia taarifa kutoka kwa raia wema 
waliowatilia shaka watu hao.
Aidha,kamishna Nzowa ameendelea kuwataka wananchi kuachana na Biashara 
hiyo haramu,ikiwa ni pamoja na kutoa wito kwa wakulima wanaozalisha 
bangi kuacha mara moja ,kwa kuwa zao hilo ni miongoni  mwa dawa za 
kulevya.Zaidi ya kilo mia tatu za Heroin zimekamatwa na kitengo  hicho 
tangu kuanza kwa mwaka huu.Hali hiyo inayopunguza kasi ya biashara hiyo 
hapa nchini.
Baadhi ya Dawa za kulevya zilizowahi kukamatwa na GODFREY NZOWA
GODFREY NZOWA(Kamishina msaidizi Mwandamizi kitengo cha kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya)
Dawa za kulevya  zilizokamatwa leo Magomeni aina ya Heroin kilo saba zenye thamani ya shilingi Bilioni 300 
Dawa za kulevya  zilizokamatwa leo Magomeni aina ya Heroin kilo saba zenye thamani ya shilingi Bilioni 300 
Mizani iliyokuwa inatumika kupimia Dawa za kulevya.
Kifaa kimojawapo ambacho wamekamatwa nacho watuhumiwa hao wa Dawa za Kulevya.
Dawa za kulevya  zilizokamatwa leo Magomeni aina ya Heroin kilo saba zenye thamani ya shilingi Bilioni 300 
GODFREY NZOWA(Kamishina msaidizi Mwandamizi kitengo cha kudhibiti na 
kupambana na Dawa za kulevya) akionyesha baadhi ya dawa za kulevya 
yaliyokamatwa.
No comments :
Post a Comment