| Bondia Pungluang Sor Singyu wa Thailand kushoto akipambana na Fadhili Majiha wa Tanzania wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Dunia WBO Asia Pacific bantamweight title uliofanyika katika uwanja wa shule ya Amphawa iliyopo Bangkok, Thailand Majiha alipigwa kwa point | 
 Na Mwandishi Wetu
BONDIA nambari moja kwa ubora nchini Tanzania katika uzito wa bantamweight
 Fadhili Majiha 'Stoper' mwishoni mwa wiki iliyopita alikuwa na kibarua 
kizito kutoka kwa Mthailand aliyemenyana nae nyumbani kwao Thailand na 
kupigwa kwa point
akizungumzia matokeo hayo ya kupigwa 
kwa point bondia huyo amejigamba na kusema kuwa yeye alistaili ushindi 
hivyo wamempa kwa kuwa kacheza kwao na mcheza kwao utunzwa mana 
nilicheza kwa ustadi wa ali ya juu na wapenzi wote wa ngumi walikuwa 
upande wangu wakitafakali kwa nini nilinyimwa ushindi
bondia huyo ambaye anatamba sana hapa 
nchini kuwa akuna wa kumbabaisha ambapo anadai kukimbiwa mara mbili na 
bondia Fransic Miyeyusho pamoja na Nassibu Ramadhani ambao wote amewapa 
onyo ole wake mmoja wao akaingia anga zake atakiona cha moto kwa kuwa 
mechi zao nyingi wanapenda kupangiana wenyewe kwa wenyewe
nimerudi nyumbani nipo fit sina ata 
kovu la aina yoyote hile hivyo nitahakikisha nafanya mazoezi kuendeleza 
ufiti niliokuwa nao na napenda kutoa tahadhali kwa bondia yoyote 
mtanzania atakayejitokeza kwa sasa mbele yangu yeye atakuwa halali 
yangu 
nae  Kocha wake Waziri Chara amejigamba kwa kusema kuwa bondia wake ni wa kimataifa ambapo michezo yake karibia mitatu kacheza 
Philippines na mwingine Thailand hivyo wao ni wa kimataifa zaidi mana mapambano aliyocheza nje yote yalikuwa magumu na raundi ni 12 ambapo zote alimaliza kwa kuwa nilimjenga katika mazingira mazuri mabondia wengi wakienda nje ya nchi wengiwao wanapigwa raundi ya kwanza ya pili awafiki ya nne
Philippines na mwingine Thailand hivyo wao ni wa kimataifa zaidi mana mapambano aliyocheza nje yote yalikuwa magumu na raundi ni 12 ambapo zote alimaliza kwa kuwa nilimjenga katika mazingira mazuri mabondia wengi wakienda nje ya nchi wengiwao wanapigwa raundi ya kwanza ya pili awafiki ya nne


No comments :
Post a Comment