Afisa
 Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama,
 akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Jangwani akiwa 
ameambatana na maafisa wenzake wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni
 shamrashamra ya maadhimisho ya miaka 69 toka Umoja wa Mataifa 
unazishwe. Kushoto kwa Bi Ledama ni Albert Okal (ILO).
************************************
Shamrashamra
 za maadhimisho ya miaka 69 toka Umoja wa Mataifa uanzishwe zimeanza 
nchini, na leo jumatano  maofisa waandamizi wa UN walitembelea shule ya 
sekondari ya Jangwani na kuwahabarisha wanafunzi hao juu ya shughuli za 
Umoja wa Mataifa hapa nchini.
Mjadala
 kati ya maofisa hao Phillemon Mutashubirwa, Programme Manager wa UN 
Habitat, Usia Nkhoma Ledama, Afisa habari wa Kitengo cha Habari cha 
Umoja wa Mataifa(UNIC), Albert Okal  (ILO),Greta Sayungi (UNICEF), 
ulijikita katika masuala ya HIV/AIDS, EBOLA, Usafi na umuhimu wakuosha 
mikono ili kujikinga na maradhi, elimu ya ujasiriamali, ajira kwa 
vijana, kazi za kujitolea, malengo ya Milenia na malengo ya Umoja wa 
Mataifa kwa ujumla wake.
Ijumaa
 wiki hii Umoja wa Mataifa utaadhimisha mkiaka 69 toka uanzishwe na 
kilele cha maadhimisho hayo yatafanyika katika viwanja vya Karimjee, 
jijini Dar es Salaam.
Afisa
 Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama 
akifafanua jambo wakati akizungumza na wanafunzi wa shule yasekondari 
Jangwani jijini Dar. Kutoka kushoto ni Phillemon Mutashubirwa (UN 
Habitat), Greta Sayungi (UNICEF) pamoja na Dr Bwijo Bijo (UNDP)
 Pichani juu na chini ni Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari 
Jangwani wakiwasiliza maafisa wa Umoja wa Mataifa waliowatembelea 
shuleni hapo.



No comments :
Post a Comment