Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Monday, March 15, 2010

CHUO KIKUU CHA AFRICA NAZARENE CHANG`ARA AFRICA CHALLENGE DHIDI YA NJALA CHA SIERRA LEONE

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

March 15, 2010

Chuo kikuu cha Kenya cha Africa Nazarene chang’ara Zain Africa Challenge dhidi ya Chuo kikuu cha Njala cha Sierra LeoneChuo kikuu cha Africa Nazarene kutoka Kenya kimeng’ara katika mashindano ya Zain Africa Challenge baada ya kuwashinda wapinzani wao Chuo Kikuu cha Njala kutoka Sierra Leone katika mashindano ya Vyuo vikuu ya Zain Afrika Challenge (ZAC) yaliyofanyika jumapili saa tatu usiku na kuonyeshwa moja kwa moja kupitia luninga ya TBC 1.
Africa Nazarene ambao walionesha umahiri mkubwa katika kujibu maswali kwa haraka haraka walipata jumla ya pointi 920 huku wapinzani wao Njala wakiambulia pointi 550.
Kufuatia ushindi huo Chuo Kikuu cha Africa Nazarene wataungana na wenzao katika raundi ya pili ya mtoano wa ZAC ambao ni chuo Kikuu cha Makerere ambao waliwashinda Chuo Kikuu cha Malawi katika ufunguzi wa mashindano hayo, pamoja na Chuo kikuu cha Ghana ambao waliwashinda Chuo kikuu cha Arusha cha Tanzania.
Vyuo Vikuu 16 vinachuana kuwania kitita cha dola za Marekani USD 50,000 pamoja na Kombe la Zain, ambayo ndiyo zawadi ya mabingwa katika msimu huu wan ne wa ZAC. Wanafunzi wa chuo kitakachoshinda watakaoshiriki katika mtoano huo pia kila mmoja wao atandoka na dola za Mareka USD 5000.
Kwa mwaka huu Tanzania inawakilishwa na Vyuo Vikuu viwili ambavyo ni Chuo Kikuu cha Tumaini pamoja na Chuo Kikuu cha Arusha. Hata hivyo Arusha tayari wamekwishatolewa, na kuwafanya watanzania sasa kuomba duha ya ushindi kwa Chuo kikuu cha Tumaini ili kiweze kufanya vizuri.
Programu ya Zain Afrika Challenge ni sehemu ya juhudi za Zain zinazolenga kuboresha sekta ya elimu na inadhihirisha dhamira ya Zain ya kuleta Ulimwengu Maridhwawa kwa wateja wa Zain.
Mwaka huu pia watazamaji wa Zain Afrika Challenge wanafursa ya kushiriki katika mchezo wa Zain kupitia SMS. Wateja wa mitandao yote nchini safari hii wataweza kujibu maswawali yanayoulizwa wakati na mtoani na kujishindia zawadi nono ambazo ni pamoja na simu mpya za mkononi aina ya Nokia N97 zenye thamani ya zaidi ya shilingi laki nane. Kushiriki katika mchezo wa ZAC watu wenye simu za mkononi watatuma majibu ya swali litakaloulizwa kwenda 15315. Zawadi hizi zitatolewa kila wiki ambapo watachaguliwa washindi watatu kila wiki.
Timu 100 kutoka Vyuo Vikuu vinavyoongoza kutoka nchi nane za Afrika ambazo ni; Tanzania, Ghana, Kenya, Malawi, Nigeria, Sierra Leone, Uganda na Zambia zilichuana katika mashindano ya awali ya kitaifa ili kutafuta nafasi ya kuwakilisha nchi zao katika mtoano wa kimataifa na kujipatia fursa ya kujishindia sehemu ya zawadi zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja (Dola za Marekani 1,000,000).
Kati ya timu hizo 100, timu 32 zilizoongoza zimefuzu kushiriki katika mashindano ya kimataifa yanayofanyika nchini Uganda katika ushindani wa hali ya juu ili kuwania nafasi ya kushiriki fainali ya mashindano ambayo yatarushwa na luninga katika nchi zote nane zinazoshiriki na pia kwa mara ya kwanza, mashindano haya yatarushwa Afrika nzima kupitia satellite ya DSTV na yatatazamwa na zaidi ya watu milioni 700 kila Jumatatu saa moja na nusu usiku kuanzia Machi 1, 2010 kwenye kituo cha Africa Magic.
Chuo Kikuu cha Makerere cha Uganda kiliuwa chuo kikuu cha kwanza kushiriki katika mashindano hayo yanayo rushwa kwa muda wa wiki 16 kikichuana na Chuo Kikuu cha Malawi.
Katika msimu wa tatu wa Zain Africa Challenge uliofanyika mwaka jana Chuo Kikuu cha Ibadan cha Nigeria kiliibua na ushindi katika mtoano huo wa chemsha bongo na kujinyakulia zaidi ya milioni 60 (USD 50, 000) kutoka Zain, wakati kila mshiriki alijipatia kitita cha dola za Marekani 5000 kila mmoja. Nafasi ya pili ilichukuliwa na Chuo Kikuu cha Kenyatta ambacho kiliondoka na dola za Marekani 35,000, na kila mshiriki dola 3,500. Vyuo vingine vyote vilivyoshiriki vilipata zawadi zenye thamani kati ya dola 5000 na dola 25,000.
Maswali katika mtoano wa ZAC yanagusa maeneo mbali mbali ikiwemo, historia, sayansi, utamaduni wa Africa, Jiographia, literature, muziki ya matukio ya wakati huo. Kadhalika ZAC huonyesha fursa zilizopo za kielemu katika Vyuo Vikuu vya Afrika kupitia video na wasifu wa wanafunzi.
Jumapili ijayo Mabingwa wa ZAC mwaka 2009 Chuo Kikuu cha Ibadan watapambana na Chuo Kikuu cha Masomo ya Maendeleo cha Ghana.

Yatakayojiri ZAC Msimu wa nne

• Kwa mara ya kwanza kutakuwa na mshindano kwa njia ya mtandao kupitia ;www.facebook.com/ILoveZainAfricaChallenge na kutakuwa na zawadi za kila wiki za dola 100 katika muda wa maongezi na zawadi ya juu itakuwa Laptop.

• Kila wiki watu watapiga kura Barani Afrika kuchagua Mchezaji wa Wiki wa Mchezo na zawadi yake ni dola za Marekani 1000.

• Watazamaji watajishindia zawadi za juu ambazo ni pamoja na simu mpya aina ya Nokia zenye intaneti, muziki na video kwa kutuma majibu ya maswali yatakayoulizwa kwenda namba 15315.

• Zain Africa Challenge sasa inajumuisha watu wetu zaidi licha ya wachezaji, watu wa Idara ya Utawala katika Vyuo Vikuu na wanavyuo kwa sababu sasa taarifa zake zinapatikana kwenye Facebook na Twitter.

No comments :

Post a Comment