Semina ya soka la wanawake iliyokuwa ikiendelea kwenye makao makuu ya shirikisho la kandanda Tanzania TFF uwanja wa karume imefikia tamati hii leo chini ya mkufunzi wa shirikisho la soka Dunia FIFA.
Akizungumza mara baada ya semina hiyo mkufunzi huyo wa FIFA MONICA STARB amesema wanawake wanaweza wakafanya vizuri katika mchezo wa soka endapop wataendelezwa.
Amesema licha ya nchi nyingi zilizoendelea haziruhusu wanawake kufanya kile wanachokipenda lakini amedai kwa kuendelea wanawake kufanya vizuri kutaendelea kufungua milango.
Ameongeza kuwa ili wanawake milango yao ya mafanikio iweze kufanikiwa wanalazimika kuyatumia vema mafunzo hayo ambayo wameyapata kwa kuinua soka la wanawake Tanzania.
Amesisitiza ni muhimu kuwepo kwa makocha wazuri wanawake lakini pia ukapewa kipaumbele mashuleni na wazazi wakahusishwa katika kuhamisisha mchezo wa soka la wanawake Tanzania.
JAB YAKABIDHI VITAMBULISHO VYA UANDISHI KWA WAANDISHI WALIOKIDHI VIGEZO VYA
KISHERIA
-
Dar es Salaam, Tanzania – Julai 2025
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB),
Wakili Patrick Kipangula, amemkabidhi rasmi ...
6 hours ago
No comments :
Post a Comment