Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, March 6, 2010

MESSI, TEVEZ KUWAJARIBU BAFANA BAFANA

Mashabiki wa kandanda wa jiji la Johannesburg watapata nafasi ya kuwashuhudia nyota wa Barcelona Lionel Messi na nyota wa Manchester City Carlos Tevez katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Afrika Kusini maarufu Bafana Bafana hapo May 27.
Timu ya taifa ya Argentina ambayo ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 walipocheza na Ujerumani, sasa kocha Carlos Alberto Parreira atakuwa na kibarua kuwakabili wa Argentina hao ambao wananolewa na nyota wa zamani wa kandanda Dunia Diego Armando Maradona.Taarifa hiyo imetolewa na chama cha soka cha Afrika Kusini Safa ukiwa ni mchezo wa mwisho wa kirafiki wa kimataifa kwa timu wenyeji hao wa fainali za Dunia.
Parreira amedai amekuwa akifurahishwa na maendeleo mazuri ya vijana wanaounda timu ya taifa ya Afrika Kusini.
Kocha huyo amesema alikwishamwambia CEO Leslie Sedibe kwamba anahitaji timu ngumu kama vile Denmark na Argentina, na siyo timu ndogo ambazo haziwezi kumsaidia kubaini mapungufu.Argentina iliichapa Germany katika uwanja wao wa nyumbani siku ya jumatano katika mchezo wa kirafiki jambo ambalo kocha Parreira kwamba anaamini wachezaji wake watakuwa na kipimo kizuri cha kubaini uwezo wao.
Argentina imepangwa kundi moja na Nigeria, Jamhuri ya Korea na Ugiriki katika kundi B na itacheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Nigeria June 12.
Bafana Bafana pia imepanga kucheza mchezo miwngine wa kirafiki dhidi ya Denmark hapo June 5 – siku tano kabla kushuka dimbani katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa fainali za Dunia ambapo watafungua na Mexico katika dimba la Soccer City hapo June 11.

No comments :

Post a Comment