Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, February 29, 2012

MEDIA DAY 2012 KUFANYIKA MACHI 24 MSASANI BEACH












WAKATI tamasha maalum kwa vyombo vya habari ‘Media Day’ kwa mwaka 2012 likipangwa kufanyika Machi 24 kwenye ufukwe wa Msasani, Kampuni ya bia Tanzania (TBL) imetoa shilingi mil.62.5 kwa ajiliya kudhamini tamasha hilo. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Uhusiano wa Jamii na Sheria wa TBL Steven Kilindo alisema kuwa wameamua kudhamini tamasha hilo kutokana na kuthamini mchango wa waandishi wa habari katika biashara za kampuni yao. Alisema kupitia udhamini wao fedha hizo zitatumika katika masuala mbalimbali hivyo watahakikisha linafanya kama ilivyokusudiwa kwani kama ilivyo lengo lake ni kuwakutanisha pamoja watu wa tasnia ya habari, kubadilishana mawazo na pia kupongezana. “TBL itahakikisha bonanza la mwaka huu litafana na litakuwa la aina yake kuanzia katika michezo, burudani, vinywaji na vyakula, hivyo tunawaomba waandishi wajitokeze kwa wingi ili kuweza kubiridika pamoja na kubadilishana mawazi,”Alisema Kilindo. Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA) ambayo ndiyo waandaaji wa bonanza hilo Juma Pinto, pamoja na kuishukuru TBL kwa udhamini huo aliiomba kutoishia kudhamini kwenye mabonanza tu bali wafanye hivyo hata katika mafunzo mbalimbali yanayoaandaliwa na chama hicho. “Tunaishukuru TBL kwa kutudhamini katika tamasha letu ambapo mmekuwa mkifanya hivyo kwa miaka kadhaa sasa, lakini tunaomba msiishie katika mabonanza tu kwani tuna semina ambazo tunaziaandaa mara kwa mara na zinahitaji kiasi kido tu cha fedha,”Alisema Pinto. Kwa upande wake Katibu Msaidizi wa Taswa, Geoge John alisema kuwa tamasha hilo litashirikisha waandishi 1500 kutoka vyombo mbalimbali vya habari ambapo kutakuwa na michezo mbalimbali itakayotangazwa baadaye pamoja na burudani ya muziki

No comments :

Post a Comment