Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, February 22, 2012

MSOND NGOMA KUTUMBUIZA MAX BAR ILALA JUMAPILI HII



BENDI kongwe ya muziki wa dansi Tanzania, Msondo Ngoma ‘Baba ya muziki’, inawaomba radhi mashabiki wao wa DDC Kariakoo kwa kuwakosa kwa wiki moja kwani kwa sasa wanapiga shoo Ya Jumapili hii watakua katika ukumbi wa Max Bar ya Ilala Bungoni Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, msemaji wa bendi hiyo, Rajabu Mhamila ‘Super D‘, alisema kuwa hawakupanga kuondoka Kariakoo lakini kutokana na muingiliano wa ratiba hawana budi kufanya hivyo ingawa wanaamini wiki zijazo mambo yatakuwa mazuri.

Alisema hata hivyo bado wanahitaji kuwa karibu na mashabiki wao kwani uwepo wao ndiyo kazi yao ya kuimba inakuwa inakamilika.

“Wiki hii hatutapiga shoo hapa Kariakoo, na tutakuwa Max bar Ilala na hii imetokana na ratiba fulani ambayo tulipewa lakini naamini wiki ijayo kila kitu kitakuwa sawa, hivyo mashabiki wetu tunaomba radhi kwa usumbufu huo,” alisema Super D.

No comments :

Post a Comment