Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt Consolata Adama akizungumza na waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusu udhamini wa kinywaji cha Grandmalt kwenye Tamasha la Sauti za Busara litakaloanza Jumatano 08/02/2012 hadi jumapili 12/02/2012 kwenye kiwanya cha Ngome Kongwe Zanzibar.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Toleo la Leo
GRAND MALT KUNOGESHA SAUTI ZA BUSARA.
Dar es Salaam, FEBRUARY 6, 2012:
Kinywaji maarufu cha Grand Malt leo kimethibitisha kukamilisha maandalizi ya kuliongezea raha tamasha la Sauti za Busara linalofanyika Zanzibar kuanzia tarehe 8 hadi tarehe 12 Februari.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa kinywaji cha Grand Malt; Bi Consolata Adam alisema; Sauti za Busara ni tamasha muhimu sana kwa nchi yetu, kwani linatangazwa ulimwengu mzima na hivyo kuvutia watu wa mataifa mbali mbali kuja kushuhudia tamasha hili, hii ni fursa kubwa kwa kutangaza vivutio vya utalii vya nchi yetu. Pia tamasha hili linaleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya muziki hapa nchini, kwa kuwaalika wasanii mbalimbali toka kila kona ya bara la Afrika, hii pia ni fursa kwa wasanii wa nyumbani kujifunza mengi toka kwa wasanii hawa.
Kufuatia umuhimu wa tamasha hili, Grand Malt imekuwa mstari wa mbele kama mmoja wa wadhamini, kuhakikisha kuwa tamasha hili litakuwa na hamasa ya aina yake, tumeweka vikundi ya kutoa burudani katika maeneo mbalimbali ambapo maandamano ya Sauti za Busara yatapita siku ya tarehe 9, ikiwemo viwanja vya Kisonge, ambapo pia wakazi wa Zanzibar watapata nafasi ya kupata kinywaji chao cha Grand Malt bila wasiwasi. Hivyo tunawakaribisha wakazi wa Zanzibar na watu wote watakahudhuria tamasha hili kuja kuburudika na Grand Malt huku tukifurahia burudani za Tamasha la Sauti za Busara 2012. Alisema Consolata.
Aidha alisema Kinywaji cha Grand Malt kitakuwa katika eneo la Ngome kongwe kwa siku zote za tamasha ili kuongeza furusa kwa watu mbalimbali kupata nafasi ya kuburudika na kinywaji kisichokuwa na kilevi na kilichotengenezwa kwa kutumia virutubisho vilivyo bora kabisa cha Grand Malt.
-MWISHO-
Kwa Maelezo zaidi wasiliana na:
Consolata Adam – Grand Malt Brand Manager, +255767266766, consolata.adam@tz.sabmiller.
Editha Mushi, Communications & Media Manager, +255767266420, editha.mushi@tz.sabmiller.com
No comments :
Post a Comment