Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza akizindua rasmi siku ya wateja wa kampuni hiyo, akiongoza wafanyakazi wenzake kuingia mitaani ili kusikiliza matatizo na kuelimisha wateja juu ya bidhaa mbalimbali za kampuni hiyo ikiwemo M-PESA na Promosheni ya Kushindania Milioni 450 zitakazoshindaniwa na wateja mbalimbali wa kampuni hiyo, katika promosheni hiyo, Wafanyakazi hao wamesambaa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kuelimisha wateja juu ya punguzo la kutuma fedha la asilimia 75 na bonasi ya asilimia 25 unaponunua muda wa maongezi kwa M-PESA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza akizungumza na wafanyakazi wenzake kabla ya kuondoka kwenda mitaani katika kuadhimisha siku ya wateja.
Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania Bw. George Rwehumbiza (kulia) akibandika Bango katika moja ya maduka ya ya Mwananyamala jijini Dar es salaam leo.
Ofisa wa Viwango na Bidhaa wa Vodacom Tanzania Elihuruma Ngowi akipata maelezo kutoka kwa Rama Juma mmoja wa wateja wa kampuni hiyo katika mduka lake huko Mwananyamala.
Mfanyakazi wa Vodacom Bw. Robert Cleofas akimpa maelezo moja ya mambango ya kampuni hiyo yenye kutoa ujumbe wa huduma za M-PESA Lina ambaye ni mfanyakazi wa Shirima Shop kabla ya kulibandika dukani hapo.
Mfanyakzi wa Vodacom George Luoga akibandika Bango lenye ujumbe wa kuelimisha huduma za M-PESA katika moja ya duka huko Mwananyamala.
Wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Vodacom wakisambaa mitaani wakati waliposhiriki siku ya wateja katika jiji la Dar es salaam na mikoa yote ya Tanzania.
Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania Bw. George Rwehumbiza akitoa maelezo kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati walipotembelea katika mitaa mbalimbali kuelimisha na kuwaelezea wateja kuhusu huduma za kampuni hiyo kuhusu M-PESA.
Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania Bw. George Rwehumbiza akitoa maelekezo kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo kabla ya kuondoka maeneo ya Mlimani City ambako ndiko ofisi zao ziliko.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akizungumza jambo na Meneja wa kitengo cha habari za Mtandao Vodacom Tanzania Matina Nkurlu.
Wafanayakazi mbalimbali wa Vodacom Tanzania wakimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza wakati alipokuwa akiongeza na wafanyakazi hao.
No comments :
Post a Comment