Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, February 7, 2012

KAMPUNI YA BIA TANZANIA (TBL) KUPITIA BIA YAKE YA SAFARI LAGER LEO IMEZINDUA RASMI MASHINDANO YA “SAFARI LAGER NYAMA CHOMA”

Meneja Masoko wa TBL,Mamongae Mahlare,Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscer Shelikindo,Jaji Mkuu wa Shindano Safari Lager Nyama Choma,Lawrence Salvi pamoja na mpiga picha wa TBC,Jane John wakila nyama choma ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa shindano hilo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscer Shelikindo akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa shindano la Safari Lager Nyama Choma ambalo linashirikisha majiko ya mabaa mbali mbali hapa nchini yanayochoma nyama.Kulia Jaji Mkuu wa Shindano hilo,Lawrence Salvi.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imezindua rasmi yale mashindano ya aina yake na ya kuvutia ya kuchoma nyama yajulikanayo kama “Safari Lager Nyama Choma”
Mashindano haya hushirikisha majiko ya baa mbalimbali katika umahiri wa kuchoma nyama na hatimaye zawadi hutolewa kwa washindi.
Akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya mwaka huu, meneja wa Bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo alisema madhumuni makubwa kwa bia ya Safari lager kuendesha mashindano haya ambayo yamekuwa kivutio kwa walaji wa nyama na watumiaji wa bia ni kuhakikisha tunaleta changamoto kwa majiko yanayochoma nyama, ili kuhakikisha walaji wanapata kile kilicho bora kabisa.
Watumiaji wa bia ya Safari Lager, hupendelea sana kuitumia huku wakisindikiza na nyama choma iliyoandaliwa vizuri, hivyo kupitia mashindano haya, bia ya Safari Lager inaendeleza utamaduni wa kunywa bia na kula nyama. Kufuatia ubora wa hali ya juu wa bia ya Safari lager, tunafurahi sana pale ambapo mnywaji atapata pia nyama iliyo bora ili mtumiaji aweze kuridhika zaidi.

Mashindano ya mwaka huu yatafanyika katika mikoa mitano ambayo ni; Dar Es Salaam, Kilimanjaro, Arusha,Mbeya.na Mwanza. Kuna ongezeko la mkoa wa Mwanza ambao mwaka juzi haukushiriki. Ni matarajio ya bia ya Safari Lager kuyapeleka mashindano haya katika mikoa yote siku za usoni.
Akitaja zawadi za washindi, Shelukindo alisema; baa itakayoshika nafasi ya kwanza itajinyakulia shilingi Milioni Moja, mshindi wa pili, Laki Nane, Mshindi wa Tatu laki Sita, Nafasi ya Nne; Laki Nne na nafasi ya Tano shilingi Laki Mbili. Zawadi hizi zimegawanywa kwa kila mkoa.
Utaratibu wa kupata baa zitakazoshiriki mashindano haya utaendeshwa kwa njia ya simu, ambapo wananchi watatakiwa kutuma ujumbe mfupi usemao “Safari kisha Mkoa uliopo ikifuatiwa na jina la Baa” kisha tuma kwenda namba 0763 514 514 Utapokea ujumbe kukuhakikishia kuwa kura yako imepokelewa.
Jopo la majaji litapitia kura zote na Baa ishirini kwa Dar Es Salaam na Kumi kwa mikoa mingine zitakazokuwa zimepata alama za juu zaidi ndizo zitakazopambana katika hatua ya pili ya tano bora ambapo majaji watazitembea tena na kutoa maksi kulingana na vigezo waliovyo navyo kasha baa hizo zitapambana katika eneo la wazi ambapo mandhari ya kula nyama na kunywa bia itakuwa imeandaliwa.

No comments :

Post a Comment