Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, February 7, 2012

JUMA NATURE, NAMELESS WAKONGA NYOYO ZA MASHABIKI DAR LIVE



MASHABIKI waliohudhuria burudani katika kituo cha maraha cha Dar Live huko Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam walipata starehe ya kutosha kutoka kwa wanamuziki Juma Kassim ‘Sir Nature’ wa hapa nchini, na Namelesa kutoka Kenya ambapo walitoa makamuzi ya nguvu usiku wa kuamkia leo.

Wanamuziki hao walitoa kauli za kuushukuru umati mkubwa uliojitokeza kwenye onyesho hilo wakisema hawakutegemea Mbagala kuwa na mashabiki wa burudani wengi hivyo.

Shoo hiyo ilisindikizwa na Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, Mashauzi Classic Band, Wakali Dancers, Zuhura na wasanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya huku washiriki wa shindano la “Cheza, Vaa Imba Kama Rihanna” wakitambulishwa kwa mara ya kwanza katika ukumbi huo. Kama anavyoonekana jukwaani mwanamuziki Nameless akitumbuiza na mmoja wa mashabiki aliyemwita apande jukwaani. Wadau wa Dar Live Wakiwa kwenye pozi la pamoja.
Wanenguaji na wanamuziki wa FM Academia wakionyesha uwezo wa nyonga zao.
Kundi zima la Wanaume Halisi likiwajibika jukwaani.
Kiongozi wa Mashauzi Classic Band, Isha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’, akinengua na mpiga gitaa wake.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Zuhura, akipagawisha mashabiki.
Mwanamuziki Ambwene Yesayah ‘AY’, akiwasalimia mashabiki.

No comments :

Post a Comment