Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, February 22, 2012

TIGO YAZINDUA PROMOSHENI YA SHINDA TIKETI

Promoshei ya shinda tiketi yako yazinduliwa leo




Taarifa kwa vyombo vya habari

Shinda tiketi
ya ndege na Tigo


22 Februari, 2012, Dar es Salaam. Tigo imeanzisha
promosheni ya kupiga simu za kimataifa ambapo mshindi mmoja atajishindia safari
ya kwenda mahali alipopiga simu zaidi kama vile Canada,China,India,Uingereza na
Marekani. Washindi wengine watajishindia begi la Tigo ambalo lina simu aina ya
Ideos,tisheti,kibebeo cha ufunguo na kalamu.

Kati ya Februari 22,2012 na
Aprili 22,2012,wateja watakao tumia zaidi ya shilingi 1,000 kupiga simu za
kimataifa wataingia moja kwa moja kwenye shindano. Jinsi unavyopiga simu za
kimataifa zaidi kwa kutumia Tigo ndivyo utakavyojiongezea nafasi ya
kushinda.

“Kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye promosheni
zilizopita,tumeamua kuwapa nafasi nyingine wateja wetu wa malipo ya kabla na
baada kujishindia zawadi nono”alisema Alice Maro ambaye ni afisa uhusiano wa
Tigo. “ Piga simu za kimataifa sasa na ushinde safari ya nje ya
nchi”

Kutakuwa na washindi 50 katika promosheni hii. Washindi 49 wa
mwanzo watajishindia begi la Tigo litakalokuwa na tisheti,kalamu,kibebeo cha
ufunguo pamoja na simu aina ya Ideos smart. Mshindi wa 50 atajishindia zawadi
kuu ambayo itakuwa ni tiketi ya ndege na fedha za kujikimu.Mshindi atapewa
maelekezo wakati wa mwisho wa maandalizi.

Tiketi ya kurudia itakuwa ni
daraja la pili (economy) na itakuwa imelipiwa ikiwa kama sehemu ya zawadi.
Tiketi itanunuliwa katika shirika ambalo litachaguliwa na Tigo. Tigo haitahusika
na ndege ambazo haijazichagua kutumika katika shindano hili.

Washindi
wote 50 watachaguliwa bila mpangilio maalum chini ya uangalizi wa msimamizi
kutoka bodi ya michezo ya bahati nasibu. Wateja watajulishwa kupitia namba
wanazozitumia kupiga simu za kimataifa. Washiriki wanatakiwa wawe na
kitambulisho halali pamoja na pasipoti wakati wanaingia kwenye shindano.
Washindi wote watazawadiwa mwisho wa promosheni.

Washiriki lazima wawe na
umri wa miaka kumi na nane na kuendelea. Shindano hili ni kwa ajili ya raia wa
Tanzania ambao ni wateja wa Tigo.

Kuhusu Tigo:

Tigo ni mtandao wa
simu za mkononi ya kwanza Tanzania, ilianza biashara mwaka 1994 na ni mtandao wa
simu Tanzania wenye ubunifu wa hali ya juu na bei nafuu kupita zote nchini. Tigo
ni sehemu ya MillicomInternational Cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za
mkononi kwa gharama nafuu na inayopatikana maeneo mengi kiurahisi kwa wateja
zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yanaoibuka Afrika na Amerika ya
Kusini.

No comments :

Post a Comment