Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
Tigo yatoa pikipiki tano kusaidia vituo vya afya Misungwi, Mwanza
06 Febuari, 2012. Mwanza. Tigo, mtandao wa simu za mkononi unaongoza Tanzania, wametoa msaada wa pikipiki tano kwa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza. Hospitali ya wilaya ya misungwi inahudumia wilaya nzima yenye wakazi zaidi ya laki tatu ambapo kwa siku hupokea wagonjwa wasiopungua 100.
Hafla ya makabidhiano ya pikipiki hizo imefanyika leo katika hospitali ya wilaya ya Misungwi.ambapo Pikipiki zimewasilishwa na Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa, Joseph Mutalemwa.
Dk. Marco Mwita Magesa ambaye ni Mganga Mkuu wa hospitali hiyo amesema pikipiki hizo zitatumika kuhudumia wagonjwa wa dharura na hivyo kusaidia kutoa tiba kwa haraka ili kuokoa maisha.
“Maeneo ya vijijini yanakabiliwa na miondombinu mibovu pamoja na ukosefu wa vyombo vya usafiri huku ukizingatia vituo vingi vya afya vipo umbali mrefu kutoka maeneo wanayoishi watu” alisema Bw. Joseph Mutalemwa.
“Pikipiki hizi ni ufumbuzi katika kukabiliana na changamoto za usafiri zinazowakabili wakazi wa wilaya hii kufikia huduma za afya kwa gharama nafuu.” aliongeza.
Naibu Waziri wa Mwasiliano Mhe. Charles Muhangwa Kitwanga alisema “Tunapenda kuwashukuru Tigo kwa mchango wa pikipiki,. Huu utakuwa ni msaada mkubwa kwa wale watakao kuwa wanahitaji huduma za afya katika hospitali hii, ningependa pia kuhamasisha makampuni mengine kufuata mfano wa Tigo katika kusaidia sekta ya afya hasa vijijini ambayo inakabiliwa na changamoto nyingi”
Pikipiki hizo zitaondoka kila siku kutumikia vituo vya afya 15 wilayani humo. Baadhi ya vitu viko umbali wa kilomita 135. Vituo vitakavyopatiwa huduma hiyo ni pamoja na Zahanati ya Mahando, Zahanati ya Mwamboku, Zahanati ya Lubili, Zahanati ya Gambajinga, Zahanati ya Nkinga, Zahanati ya Mwawile, Kituo cha Afya cha Busongo, Kituo cha Afya cha Koromije, Zahanati ya Idetemya, Kituo cha Afya cha Misasi na Kituo cha Afya cha Ikungumhulu.
Pikipikia zitarudi siku hiyo hiyo zikiwa na sampuli katika mifuko maalumu inayozuia joto na mtikisiko. Wagonjwa ambao walikuwa wanasubiri kwa miezi kupata matokeo yao sasa watapata katika siku chache tu
“Lengo la msingi ni kuboresha upatikanji wa huduma za afya wakati wa kujifungua, hasa inapotokea dharura katika huduma za uzazi kuwasaidia wanawake na watoto wao kupata matibabu baada ya kujifungua,” alisema Dk. Marco Mwita. “Pikipiki hizo zitatumika kusafirisha wanawake waliopata matatizo baada ya kujifungua kama vile kutokwa na damu, kubaki kwa nyumba ya mtoto, fistula pamoja na ajali za barabarani,” alisema.
Magonjwa mengine ya kuwaida yanayotibiwa katika kituo hicho ni gastroenteritis, pneumonia, malaria, maambukizi ya njia ya mkojo (UTI), maambukizi katika mfumo wa juu wa upumuaji., kuharisha kwa watoto ,magonjwa ya ngozi, maambukizi ya jicho ikiwa ni pamoja na kiwambo ute cha jicho, bacteria kuhara damu pamoja na homa ya matumbo.
Bw. Mutalemwa amesema Tigo ni kampuni inayowajali wateja, na anahamasisha watu kutumia bidhaa na huduma bora za Tigo ambazo zinapatikana kwa bei nafuu nchini kote.
Chini ya mkakati wake wa maendeleo jamii, Tigo inalenga kusaidia kuboresha maisha ya wakazi kwa kuendeleza mikakati ya kudumu y enye dhima tatu za kimataifa elimu, mazingira na maisha bora.
Kuhusu Tigo:
Tigo ni mtandao wa kwanza wa simu za mkononi Tanzania, ilianzishwa mwaka 1994, ni mtandao wa simu unaongoza kwa ubunifu wa hali ya juu na ni wa bei nafuu kupita zote nchini. Tigo ni sehemu ya MillicomInternational Cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za mkononi kwa gharama nafuu na inapatikana maeneo mengi kiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yaliyoko Afrika na Amerika ya Kusini.
Msingi wa mafanikio ya Tigo ni uzingatiaji wa mikakati mitatu ambayo ni Gharama nafuu, Uwepo na Upatikanaji .Tunajenga dunia ambapo huduma za simu ni za bei nafuu, zipo na zinapatikana kila mahali na kwa wote. Hii inahakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma bora zaidi kwa bei nafuu kuliko zote katika mikoa yetu 26, Tanzania Bara na Zanzibar.
Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz
Imetolewa na:
Alice Maro • PR-Tigo • Simu 255 715 554501
No comments :
Post a Comment