Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, February 21, 2012

HATIMAYE WAZIRI NCHIMBI AWAPATANISHA RUGE NA SUGU

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba wakipeana mikono leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni ishara ya kupatana na kumaliza kwa tofauti zao zilizotokana na sababu za kimuziki zilizodumu kwa muda wa miaka miwili. Huku wapatanisha wa mgogoro huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu (kulia) wakishuhudia. (Picha na Anna Nkinda - Maelezo)

Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba (kulia) akimsikiliza Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao uliotokana na sababu za kimuziki uliodumu kwa muda wa miaka miwili. Wapatanishi wa mgogoro huo ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na kumalizika kwa mgogoro wa miaka miwili uliotokana na sababu za kimuziki baina ya Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Katikati) na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba (kulia). Wapatanishi wa mgogoro huo ni Waziri Dk. Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam juu ya mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao uliodumu kwa muda wa miaka miwili. Wapatanishi wa mgogoro huo ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu..

No comments :

Post a Comment