Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, February 7, 2012

TWANGA ACADEMIA TAYARI KUANZA KAZI



Mkurugenzi wa Kampuni ya The African Stars Entertainment (ASET), Asha Baraka akiwa na Mwanamuziki Mkongwe nchini,Mzee Hamza Kalala.
Mkurugenzi wa Kampuni ya The African Stars Entertainment (ASET), Asha Baraka, akionesha vifaa vya muziki vitakavyotumiwa na Taasisi ya kuvumbua vipaji ya Twanga Academia wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya The African Stars Entertainment (ASET), Asha Baraka, akionesha vifaa vya muziki vitakavyotumiwa na Taasisi ya kuvumbua vipaji vya wapigaji ala za muziki ya Twanga Academia wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Kushoto ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Warren Reed.
MKURUGENZI wa Kampuni ya The African Stars Entertainment (ASET), Asha Baraka, ametangaza kutoka kivingine kwa kuanzisha Taasisi ya kuvumbua vipaji itakayokwenda kwa jina la Twanga Academia.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, alisema kwamba, Twanga Academia tayari wamenunua vifaa vyenye thamani ya sh. milioni 100 kwa kuanzia.

Aidha, aliongeza kuwa, wamepanga kufanya usaili wa kusaka vipaji mbalimbali vya muziki, Jumapili ijayo Februari kwenye viwanja vya Leaders Club, kuanzia saa 6:00 mchana.

Asha aliongeza kuwa, usaili huo, utasimamiwa na magwiji wa muziki wa dansi, kama Hamza Kalala ‘Komandoo au Mzee wa Madongo’, Rais wa FM Academia, Nyoshi El Saadat na wengineo kadhaa, ambako watatoa fursa kwa chipukizi wanye uwezo wa kutumia ala za muziki.

“Lengo la Twanga Academia, ni kusaka vipaji vya waimbaji, pamoja na wanamuziki wenye uwezo wa kupiga ala, ambavyo vitaendelezwa kwa kupitia wakufunzi watakaowafunda mara baada ya kupatikana,” alisema Asha.

Kwa upande wake, Mkongwe Komandoo Kalala, alimpongeza Asha kwa hatua hiyo aliyofikia na kwamba, ndiye atakuwa wa kwanza kukumbuka kuvumbua vipaji vya wapigaji wa ala za muziki.

“Hiki kitu mimi nilikuwa nakizungumzia kila siku, kwani ni wanamuziki wachache sana, ambao wanajua kuimba na kutumia ala, wengi ni washika vipaza sauti tu, mambo mengine hawajui, lakini hawajachelewa wanaweza kuanza sasa, kwani elimu haina mwisho,” alisema Kalala.

Aliongeza kuwa, binafsi anamuunga mkono Asha, kutokana na kuja na wazo hilo jipya.

“Tunaliheshimu wazo lake jipya alilokuja nalo na tutaitumia nafasi hiyo, kwa kuwapa elimu wanamuziki chipukizi ili kuongeza tija kwa wapiga ala, tofauti na ilivyo hivi sasa,” alisema.

Alitoa wito kwa wazazi na walezi, kuwapa ruhusa vijana wao kwenda katika usaili siku hiyo itakapofika.

Mbali ya kusaka wanamuziki watakaomudu kupiga ala, pia watakaojitokeza watafundishwa kuimba na kucheza, ambako zoezi hilo pia linawahusu wasanii wa mikoani hivyo wajitokeze

No comments :

Post a Comment