Meneja Mwendeshaji wa Kampuni ya Integrated Communications Ltd ambao ni waratibu wa kampeni hiyo nchini,Laurance Andrew akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu maendeleo ya programu ya wezeshwa yenye lengo la kutoa ruzuku kwa wamiliki wa biashara ndogondogo nchini Tanzania ambapo jumla ya kiasi cha shilingi milioni mia mbili (200,000,000) zitatolewa na mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni 02/03/2012.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza maendeleo ya kampeni ya aina yake ya kuwatafuta na kuwawezesha wajasiriamali wadogowadogo katika shindano la wezeshwa na Safari Lager na unaweza kupata ruzuku ya kusaidia kuona njia ya mafanikio katika mikoa ya Mwanza,Mbeya na Arusha ambapo sasa zimesalia siku 21 kabla ya zoezi hilo kufungwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dasr es salaam,Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema Bia ya safari Lager ilizindua program maalum ya kuwawezesha ya kufanikisha kuwawezesha wajasiriamali wadogowadogo nchini kupitia programu ya wezeshwa na Safari lager Novemba 24 jijini Dar Es Salaa ikiwa na lengo kuu la kuwasaidia wamiliki wa biashara ndogondogo na za kati kukuza biasharazao.
Alisema programu hiyo ilizinduliwa katika kanda kuu nne za Tbl ambazo ni kanda ya Dar Es Salaa,Kanda ya Ziwa,kanda Kaskazini na kanda ya nyanda za juu kusini ambapo wamiliki wa biashara ndogondogo walipaswa kuchukua fomu maalum toka katika bohari na viwanda vya Tbl katika mikoa yao au pia kuchukua fomu kwenye tovuti www.wezeshwa.co.tz au kutuma barua pepe kwenda info@wezeshwa.co.tz au unaweza kupiga simu nambari 0763 600041 (Dar es Salaam) 0763600042 (Arusha) 0763 600044 Mwanza) na 0763 600045 (Mbeya) namwishowakurudishafomuni 02 Machi 2011
Alisema kwa hivi sasa programu hiyo inaelekea ukingoni ambapo hivi karibuni jopo la majaji walibobea katika elimu ya uendeshaji wa biashara wataanza mchakato wa kupitia fomu zote zilizotumwa ili kuweza kupata washindi kwa kila kanda.
Leo hii tunapenda kuwafahamisha watanzania kuwa zimebaki takribani majuma matatu kabla ya pazia la kuchukua na kurejesha fomu kufungwa rasmi tarehe 02.03/2012 saa sita usiku hivyo napenda kuchukua nafasi hii kuwakumbusha wale wamiliki wa biashara ndondogo waliochukua fomu kurejesha katika vituo husika mapema na pia kwa wale ambao bado hawajachukua maamuzi ya kushiriki kufanya maamuzi hivi sasa maana muda umebakia mchache sana na kama tunavyofahamu sote Safari Lager imeandaa kiasi cha Shilingi milioni mia mbili ( 200,000,000) ambazo zitatolewa kwa wamiliki wa biashara kama ruzuku na pia wataalamu wetu watafanya mchakato wa kuwawezesha hao washindi ishirini kwa kila kanda kuweza kuwapatia semina na elimu ya ujasiriamali na namna ya kuendeleza na kukuza biashara zao,Alisema bwana Shelukindo
No comments :
Post a Comment