Matroni wa Haopitali ya Temeke jijini Dar es Salaam, akitoa
ukaribisho kwa wageni mbalimbali waliofika katika hafla ya kupokea msaada wa
vifaa mbalimbali vya Hospitali ya Temeke na Buguruni Vilivyotolewa na Benki ya
KCB Tanzania vikiwa na thaman ya shilingi milioni 17,152,000.
Mkurugenzi
wa Bodi wa Benki ya KCB Tanzania Mama Zuhura Muro,(kulia) akimkabidhi Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam, DR.Amani Malima,mashine
ya kumsaidia mgonjwa kupumulia wakati wa hafla ya kukabidhiwa vitu mbalimbali
kwa ajiri ya Hospitali ya Temeke na Buguruni vyenye thamani ya shilingi Milioni
17.152.000.(katikati) Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Temeke James Magoti.
Mkurugenzi wa Bodi wa Benki ya KCB Tanzania Mama Zuhura
Muro,(kulia) akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke jijini Dar es
Salaam, DR.Amani Malima,akimkabidhi msaada wa Folding Screens moja kati ya 3
zilizotolewa msaada na benki hiyo ikiwemo vitu mbalimbali vyenye thamani ya
shilingi milioni 11,152,000 ka ajiri ya hospitali hiyo. (Kulia) Mwenyekiti wa
Bodi ya Hospitali ya Temeke James Magoti.
Wafanyakazi wa benki ya KCB Tanzania wakiongozwa na
Mkurugenzi wa Bodi wa Benki ya KCB Tanzania Mama Zuhura Muro, wakiwa katika
picha ya pamoja na wafanyakazi wa Hospitali ya Temeke na Buguruni zote za
jijini Dar es Salaam, baada ya KCB kukabidhi Msaada wa vifaa mbalimbali kwa
hospitali hizo wenye thamani ya shilingi Milioni 17,152,000.
Na Mwandishi wetu
Benki
ya KCB Tanzania, imetoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya kusaidia afya ya
mama na mtoto vyenye thamani ya shilingi 17,152,000/- kwa hospitali za Temeke na
Buguruni zilizopo jijini Dar es Salaam
Akizungumza
katika hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo iliyofanyika jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki, mkurugenzi wa bodi ya benki hiyo Zuhura Muro alisema
katika kuhadhimisha wiki ya jamii mwaka huu benki ya KCB imeamua kuelekeza
misaada yake katika sekta ya afya
“Wakati
wa wiki ya jamii mwaka jana na juzi tulitoa madawati na vitabu kwa shule
mbalimbali nchini. Mwaka huu tumechagua kusaidia sekta ya afya hasa kwa upande
wa akinamama na watoto ili kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na uhaba wa vifaa
muhimu hospitalini,”
“Mkurugenzi
huyo wa bodi alisema benki ya KCB inaatambua umuhimu wa afya ya mama na mtoto na
ndiyo maana tumeona ni jambo zuri kuwekeza katika sekta ya afya. Nikiwa kama
mama ninayo furaha kwa kuwa naamini msaada huu utaweza kuokoa maisha ya akina
mama na watoto,” alieleza
Kwa
upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya Temeke Amani Malima alisema kuwa
hospitali yake imekuwa ikihudumia akina mama wengi kuliko uwezo wake kutokana
ukosefu wa vifaa.
“Tunapokea
akina mama wengi wanaokuja kujifungua zaidi ya uwezo wetu. Wengine huwa
wanazaliwa wakiwa bado hawajatimia na hulazimika kuwapa rufaa ya kwenda
hospitali nyingine kama Muhimbili kutokana na kutokuwa na vifaa. Tunaishukuru
benki ya KCB kwani msaada huu utasaidia kuboresha hali,” alisema
Naye
mganga mfawidhi wa hospitali ya Buguruni Dr Hawa Lesso aliishukuru benki ya KCB
na kusema kuwa utasaidia kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa kabla wakiwa
hawajatimia (pre mature).
Watoto
wanaozaliwa kabla ya kutimia wakati mwingine hupoteza maisha kabla ya kuwapa
rufaa ya kwenda hospitali nyingine kutokana na ukosefu wa vifaa. Tunaishuru
benki ya KCB kwani imesikiliza kilio chetu, Tunaomba taasisi nyingine za kifedha
kuiga mfanio wa benki ya KCB.
Vifaa
vilivyotolewa kwa hospitali ya Temeke ni pamoja na mashine moja ya joto kwa
watoto waliozaliwa bila kutimia (Incubator), Folding screens 10, seti ya mashine
ya hewa 3 (Oxygen flow meter) na sare za wauguzi pea 10 vyote vikiwa na thamani
ya shilingi 11,252,00/-
Hospitali
ya Buguruni ilipokea mashine moja ya joto kwa watoto waliozaliwa bila kutimia
yenye thamani ya shilingi 5,900,000/-
No comments :
Post a Comment