AIRTEL YAKABIDHI T-SHIRT 400 NA MILIONI TANO KWA AJILI YA MASHINDANO YA RIADHA YA ROCK CITY
Ofisa
Uhusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Bi Jane Matinde (kulia)
akimkabidhi moja kati ya T-shirt mia nne Meneja Matukio wa kampuni ya
Capital Plus International ambaye pia ni Mratibu wa mbio za Rock City
Marathon za mwaka huu, Bi Grace Sanga jijini Dar es Salaam jana kama
sehemu ya udhamini wa mbio hizo zitakazofanyika katika uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza tarehe 28 Oktoba. Airtel walikabidhi T-shirt mia
nne pamoja na milioni tano kusaidia mbio hizo. Ofisa

akimkabidhi hundi ya shilingi milioni tano Meneja Matukio wa kampuni ya
Capital Plus International ambaye pia ni Mratibu wa mbio za Rock City
Marathon za mwaka huu, Bi Grace Sanga jijini Dar es Salaam jana kama
sehemu ya udhamini wa mbio hizo zitakazofanyika katika uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza tarehe 28 Oktoba. Airtel pia walikabidhi T-shirt
mia nne zitakazotumika katika mbio hizo. AIRTEL yaahidi kuendelea kusaidia maendeleo ya michezo nchini KAMPUNI
ya mawasiliano nchini ya Airtel imeahidi kuendelea kusaidia michezo
mbalimbali nchini ikiwa na lengo la kukuza maendeleo ya vijana.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana katika hafla fupi ya kukabidhi
shilingi milioni tano pamoja na T-shirt mia nne kama udhamini wa mbio za
Rock City Marathon za mwaka huu zenye kauli mbiu ‘tukuze utalii wa
ndani kupitia michezo’, Afisa Uhusiano wa Airtel, Bi Jane Matinde
alisema kuwa kampuni yake itaendelea kusaidia michezo mbalimbali nchini
ikiwemo riadha ili kukuza maendeleo ya vijana.
“Udhamini wetu wa shilingi milioni tano pamoja na T-shirt mia nne
katika mbio za Rock City mwaka huu unalenga katika kusukuma maendeleo ya
vijana kupitia michezo kwa kuwa tunaamini kuwa michezo imekuwa ni
chanzo kikubwa cha ajira duniani.
“Tunaahidi kuendelea kusaidia michezo mingine kwa kuwa pia tunaamini
kupitia michezo mbalimbali tunaweza kutangaza vivutio vyetu vya utalii
duniani. Mfano nzuri ni mbio za mwaka huu za Rock City Marathon
zitakazowakutanisha wanariadha mbalimbali kutoka nchi jirani,” aliongeza
Bi. Matinde.
Akipokea hundi na T-shirt hizo, Mratibu wa mbio hizo kutoka katika
kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bi. Grace Sanga aliishukuru
kampuni ya Airtel kwa kuendelea kusaidia mbio za Rock City na kuyahasa
mashirikia na makampuni mengine kuiga mfano wa kampuni hiyo.
“Tunaishukuru Airtel kwa msaada wao kwa kuwa msaada huu utatusaidia
tujiandae vizuri na Rock City Marathon ya mwaka huu itakayofanyika
Oktoba tarehe 28 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza,” alisema
Grace.
Grace alisema kuwa mbali na Airtel wadhamini wengine ni pamoja na
Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Parastal Pension Fund (PPF), Geita
Gold Mine, African Barrick Gold, Air Tanzania Company Ltd (ATCL),
Mamlaka ya Taifa ya Mbuga za Wanyama nchini (TANAPA), Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB), Nyanza Bottles, New Africa Hotel na New Mwanza Hotel.
Aidha, Bi Sanga aliwaasa wanariadha kujitokeza na kuanza kujisajili ili
kushiriki katika mbio hizo na kusema kuwa fomu za usajili zinapatikana
katika ofisi za uwanja wa CCM Kirumba, ofisi za kampuni ya Capital Plus
International zilizopo katika jengo la ATCL ghorofa ya tatu, ofisi za
Bodi ya Utalii jengo la IPS ghorofa ya tatu, Dar es Salaam, na
zinapatikana katika tovuti ya www.rockcitymarathon.blogspot.com.
CPI ilitangaza kuwa atakayeibuka kinara katika mbio za kilometa 21
mwaka huu kwa wanaume na wanawake atazawadiwa shilingi milioni moja na
laki mbili wakati mshindi wa pili ataweka mfukoni shilingi laki tisa na
mshindi wa tatu ataondoka na shilingi laki saba.
No comments :
Post a Comment