Meneja
mauzo wa Kinondoni na Ilala wa Kampuni ya Bia Tanzania, Victor Kavishe
(wa pili kushoto) akimkabidhi Kikombe nahodha wa Klabu ya Lugalo,
Eliutha Shawa mara baada ya kuibuka mabingwa wakati wa mashindano Safari Darts kwa Vilabu vya Mkoa wa Dar es Salaam.Kushoto ni Mwenyekiti wa Darts Mkoa wa Dar es Salaam.
KLABU ya Lugalo ya mchezo wa vishale ya jijini Dar es Salaam, ilifanikiwa
kutwaa ubingwa wa mashindano ya vishale yaliyojulikana kwa “Safari
Darts Dar Clubs Championship 2012” kwa kushilikisha vilabu kumi vya
mchezo huo vya jijini Dar es Salaam kwa pointi 18 mwishoni mwa wiki.
Lugalo
walitwaa ubingwa huo na kuzawadiwa Kikombe na pesa taslimu shilingi
laki tatu na Meneja mauzo wa Kinondoni na Ilala, Victor Kavishe ambaye
alikuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo.
Mshindi
wa pili katika mashindano hayo ni klabu ya Upanga ambayo ilipata
pointi 16 na wa tatu ni Polisi Balax ambao walipata pointi 13.
Mashindano hayo yaliendeshwa kwa mfumo wa ligi mpaka washindi kupatikana na vilabu vilivyoshiliki ni Lugalo, Upanga,Polisi Balax,Freinds,Magereza,Mbezi Beach,Kashudu,Kawe na Kimanga.
Akizungumza
na waandishi wa habari Meneja mauzo wa Kinondoni na Ilala wa TBL,
Victor Kavishe alisema kampuni ya Bia ya Safari Lager iko bega kwa began
a mchezo wa Darts kuhakikisha inasaidia kwa kila linalowezekana
kuendeleza na kukuza mchezo huo hapa nchini na pia aliwapongeza
washiriki wote kwa utulivu mpaka washindi kupatika kkwa amani na
aliwapongezwa washindi Lugalo kwa kutwaa Ubingwa ambao pia walikuwa
washindi wa pili katika mashindano ya mchezo huo ya Afrika mashariki
yaliyomalizika hivi karibuni.
Nae
katibu wa Darts Mkoa wa Dar es Salaam, Lambarth Rwihula aliishukuru
Kampuni ya Bia ya Safari Lager kwa ufadhili wao na kuwaomba makampuni
mengine waige mfano huo.
No comments :
Post a Comment