Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, September 28, 2012

SUPER SPORT KUITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA KATIKA MEDANI YA MICHEZO KWA KUZINDUA WIKI YA SOKA TANZANIA





Meneja Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Peter Fauel akifafanua ujio wa Super Sport nchini Tanzania na kuipongeza TFF kwa kuonyesha ushirikiano na kuwa Chaneli hiyo itaonyesha mechi tano za Ligi ya Tanzania kuanzia leo Ijumaa hadi Jumatano Oktoba 3 mwaka 2012.
Mkuu wa Super Sport barani Afrika Bw. Andre Venter akielezea furaha yake kuja Tanzania na kupata fursa ya kulitangaza soka la Tanzania kimataifa kupitia chaneli ya Super Sport amesema chaneli hiyo imechafanya kazi katika nchi za Kenya na Uganda na Sasa ni wakati wa Tanzania kuonyesha kiwango chake cha soka Kimataifa.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini (TFF) Bw. Leordiga Tenga akitoa nasaha zake wakati wa uzinduzi wa wiki ya Soka Tanzania ambapo amevitaka vilabu vitakavyopata bahati ya kuonekana katika chaneli hiyo kuonyesha kiwango cha soka la Tanzania na kuzingatia nidhamu haswa mechi ya Watani wa Jadi Yanga na Simba ambao wanatambulika barani Afrika kama timu zenye upinzani mkali.
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Bi. Furaha Samalu akifurahi jambo na watangazaji wa kipindi cha Africa Soccer Show wakati wa halfa hiyo.
Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo kuwa Super Sport wakishirikiana na TFF wapo hapa nchini na kwa mara ya kwanza wanaonyesha mechi za Ligi ikiwemo timu ambazo hata siku moja hazijawahi kuonekana kwenye Chaneli ya Super Sport na kuwataka wachezaji wa timu hizo kuonyesha uwezo wao kwa sababu ni fursa ya pekee kuonekana katika nyanja ya Kimataifa. Aidha amewataka Watanzania ambao hawajaunganishwa na DStv wafanye hima kununua ving'amuzi ili waweze kushuhudia mechi hizo pamoja na chaneli nyinginezo zinazopatikana katika DStv.
Meneja Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Peter Fauel akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla fupi ya uzinduzi wa wiki Soka Tanzania iliyofanyika jijini Dar kwenye Hoteli ya Southern Sun.
Dada Levina kutoka Multichoice Tanzania anayetazama kamera akifurahi jambo na wadau.
Meneja fedha wa Multichoice Tanzania Bw. Senguti (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Peter Fauel.
Baadhi ya Wadau wa michezo wakipata viburidisho wakati wa uzinduzi wa wiki ya soka Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Peter Fauel (katikati) katika tete- a -tete na Rais wa TFF Bw. Leordiga Tenga na Mkuu wa Super Sport Afrika Bw. Andre Venter.

No comments :

Post a Comment