Warembo
wanaowania taji la Redd’s wakiwa mazoezini jana kwenye Club ya TCC
Chang’ombe jana. Shindano hilo litafanyika Ijumaa hii Sept 21, kwenye
ukumbi wa PTA(Sabasaba Hall).(Picha na Intellectuals Communications
Limited)
Warembo
wanaowania taji la Redd’s litakalofanyika Ijumaa hii Sept 21, kwenye
ukumbi wa PTA(Sabasaba Hall), wakiwasiliza wakufunzi wao kutoka kulia
Joyce Maweda, Leyla Bhanji, Hawa Ismail na Mwajabu Juma wakati wa
mazoezi yao jana kwenye Club ya TCC Chang’ombe.(Picha Intellectuals
Communications Limited)
Kamati ya Redds Miss
Tanzania leo inatarajiwa kutembelea kambi ya Redd’s Temeke 2012, kubwa
ni kuwafunda vimwana hao kutoka Vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na
Chang’ombe, kuhusu mambo mbalimbali ndani ya mashindano ya urembo.
Kamati
hiyo itaongozwa na Mkurugenzi wake, Hashim Lundenga atakayefuatana na
mshauri wa masuala ya urembo katika kamati yao, Dk. Ramesh Shah, katibu
Bosco Majaliwa, Mkuu wa Itifaki, Albert Makoye na mjumbe wa kamati hiyo,
Lucas Rutta.
Shindano
la Redd’s Miss Temeke, linafanyika Ijumaa hii katika ukumbi wa
PTA(SabaSaba Hall) na tiketi za VIP zimeshaanza kuuzwa katika Club za
City Sports Lounge iliyopo makutano ya Samora na Azikiwe na Nyumbani
Lounge iliyopo maeneo ya Namanga ambapo VIP kwa mtu mmoja ni Tshs 50,000
na pia waweza nunua kwa meza moja ama ya watu 8 kwa laki 4 au watu kumi
laki 5.
Warembo
hao ni Agness Goodluck, Angela Gasper, Flaviana Maeda,Edna Sylvester,
Catherine Masumbigana, Khadija Kombo, Neema Doreen, Flora Kazungu,
Lilian Joseph, Elizabeth Peter, Elizabeth Boniphace, Jesca Haule, Zulfa
Bundala, Mariam Ntakisivya na Esther Albert.
Mbali ya vinywaji vya Redd’s na Dodoma Wine, Miss Temeke pia imedhaminiwa na gazeti la Jambo Leo, katejoshy.blogspot.com,
Mariedo Boutique, Push Mobile, City Sports Lounge, 100.5 Times FM,
Kitwe General Traders, Global Publishers na 88.4 Cloud’s FM.
Shindano
hili litakuwa ni miongoni mwa mashindano ya lala salama kabla ya kupata
warembo watakaoungana na warembo wa kanda nyingine kuingia kambini
kumtafuta mrembo wa Redds Miss Tanzania kwa Mwaka huu.
No comments :
Post a Comment