Mtaalamu wa Biashara na Masoko wa
Tigo Gaudence Mushi (kulia), ambao ni wadhamini wa Maonyesho ya sarakasi
ya Tigo Mama Afrika akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
alisema watazamaji wajitokeze kwa wingi ili waweze kupata burudani ya
aina yake itakayowaacha katika hali ya furaha. Maonyesho ya mwaka huu
hayatakuwa tu bora bali pia yatakuwa ni maonyesho ambayo yanatukuza na
kuunga mkono sanaa na utamaduni wa Tanzania kitu ambacho tunaamini
kitawatia moyo watu wengine kufanya hivyo. Pembeni yake ni Mkurugenzi
wa Mancom Centre, Constantine Magavilla pamoja na Afisa habari wa Tigo
Alice Maro.
Mkurugenzi wa Mancom Centre,
Constantine Magavilla (kati) akiongea mbele ya waandishi wa habari
kuzunguzia maonyesho yanayotarajia kuanzia Alhamis tarehe 27 Septemba
2012 mpaka Jumapili Novemba 4, 2012 maonyesho ya sanaa ya sarakasi
yatafanyika katika ukumbi wa Mancom Centre New world Cinema Mwenge, Dar
es Salaam yakiambatana na programu ya nyimbo za kitamaduni na za
kisasa, upindaji wa viungo, michezo ya viinimacho, michezo ya angani,
michezo ya piramidi, michezo ya ufito na boriti na mingineyo mengi.
“Tunapenda kuwashukuru Tigo kwa
mchango wao mkubwa na kututia moyo katika maandalizi ya maonyesho haya,”
alisema Constantine Magavilla Mkurugenzi wa Mancom Centre. “Tunatumaini
kuwa watu hawataondoka hapa wakijisikia tu vizuri bali pia watakuwa
wajumbe wazuri kwa watu wengine ili kuwashawishi wengine waje kufurahia
maonyesho haya,” alisema.
Waandishi wa habari wakionyeshwa
ukumbi utakaofanyiwa maonyesho hayo. Maonyesho ya sarakasi ya Mama
Afrika yalianzishwa mwaka 2003 kama shule ndogo ya sarakasi na bwana
Winston Ruddle aliyekuwa Mkurugenzi na mwaanzilishi . Maonyesho ya
sarakasi ya Mama Afrika yamekua na kuwa moja ya maonyesho makubwa yenye
gumzo na vipaji vya sarakasi na kutoa fursa ya kutambulisha kikundi
maarufu kutoka bara la Afrika, ‘Hakuna Matata Acrobats.’
Moja ya michezo ya wanyama Mamba
itakayoonyeshwa katika maonyesho hayo. Tiketi zinapatikana sasa na
zinaweza kununuliwa katika ukumbi wa Mancom ndani ya Centre New World
cinema Mwenge, watazamaji watakuta mpangilio wa viti uliopangwa
kutokana na bei za tiketi utakaowaongoza wao kuchagua tiketi ya
kununua na idadi ya tiketi wanazohitaji. Bei ya tiketi inaanzia 10000
na muda wa maonyesho ni saa 9:30 mchana na saa 2:00 kamili usiku, Mara
tano kwa wiki.
No comments :
Post a Comment