Redd's
Miss Temeke 2012, Edda Sylivester (katikati) akipunga mkono kwa furaha
akiwa na washindi wenzake mshindi wa pili Catherine Masumbigana
(kushoto) na Flaviana Maeda (kulia) mara baada ya kutangazwa washindi
katika shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa
PTA, jijini Dar es Salaam.
*********************************
Edda
ambaye ametokea katika shindano la kitongoji cha Kigamboni ataungana na
Flaviana Maeda kutoka Kurasini ambaye amenyakuwa nafasi ya pili na
kujichukulia kitita cha shilingi 800,000.
Mrembo Catherine Masumbigana amechukua mshindi wa tatu katika shindano hilo na kujinyakulia kitita cha shilingi 700,000.
Warembo
hao watatu wamepata nafasi ya kuingia katika kambi ya Redd's Miss
Tanzania ambayo itashirikisha jumla ya warembo 30 ambao watakaa kambini
kwa muda wa mwezi mmoja.
Warembo
Jesca Haule ambaye alishika nafasi ya nne amejipatia kitita cha
shilingi 400,000 na nafasi ya tano ilienda kwa Agnes Gudluck ambae
amejipatia shilingi 300,000.
Washindi
wote watatu kila mmoja atajipatia nguo ya kutokea jioni sanjari na
viatu, vikiwa na thamani ya kila mmoja shilingi 500,000 kutoka katika
Duka la kisasa la Mariedo Boutique itatoa gauni la Sh.350,000 na kiatu
cha Sh 150,000
kila mmoja kwa washindi hao watatu wa kwanza watakaoshinda.
Warembo
wengine ambao walishiriki kutoka katika vitongoji vya
Kurasini,Kigamboni na Chang'ombe ambao ambao wameambualiwa kifuta jasho
cha shilingi 200,000 kila mmoja ni Angela Gasper, Khadija Kombo, Neema
Doreen, Flora Kazungu, Lilian Joseph, Elizabeth Peter, Elizabeth
Boniphace, Zulfa Bundala, Mariam Ntakisivya na Esther Albert.
Katika
shindano hilo washehereshaji walikuwa wasanii wanaong’ara katika
luninga, Mpoki wa kundi la Komed Original na Steve Nyerere ambao
walionekana kuvunja mbavu za mashabiki waliyoudhulia shindano hilo.
Licha
ya kuwepo kwa Mpoki na Steven Nyerere Bendi ya muziki Mashujaa
Wanakibega ambao waliweza kutoa burudani ya nguvu chini ya Rais wao
Charles Baba.
Taji
la Redd's Miss Temeke, linashikiliwa na mrembo Husna Twalib. Warembo wa
Miss Temeke wamekuwa wakijifua kwa wiki tatu sasa chini ya ukufunzi wa
Leyla Bhanji, ambaye amekuwa akisaidiwa pia na warembo wa miaka ya nyuma
wa Miss Temeke akiwemo, Regina Mosha(20020, Hawa Ismail(2003),
washiriki wa mwaka jana Joyce Maweda, Mwajabu Juma, Cynthia Kimasha na
katika shoo wamekuwa na Dickson Daud kutoka kundi la THT.
Mbali
ya Redd's, Miss Temeke 2012 pia imedhaminiwa na City Sports Lounge,
Jambo Leo, Mariedo Boutique, Global Publishers, Dodoma Wine, Push
Mobile, Mariedo Boutique, 100.5 Times FM, Kitwe General Traders, Fredito
Entertainment, katejoshy.blogsport.com na 88.4 Cloud's FM.
Temeke
imewahi kutwaa taji la Miss Tanzania mara tatu, kupitia warembo
Happiness Sosthenes Magesse aka Millen mwaka 2001, Sylvia Remmy Baham
mwaka 2003 na Genevieve Mpangala. Lakini pia imetoa warembo waliowahi
kushika
nafasi ya pili na tano bora katika Miss Tanzania kama Jokate Mwegelo,
Irene Uwoya, Irene Kiwia, Queen David, Cecylia Assey, Sabrina Slim,
Miriam Odemba, Ediltruda Kalikawe na Asela Magaka
No comments :
Post a Comment